Don't Look Back (Heroes)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
"Don't Look Back"
Sehemu ya Heroes
Heroes s01e02.jpg
Hiro Nakamura akitangaza "Yatta!" = "ameweza" kufika kwenye Times Square, New York.
Sehemu ya. Msimu 1
Sehemu 2
Imetungwa na Tim Kring
Imeongozwa na Allan Arkush
Tayarisho la 102
Tarehe halisi ya kurushwa 2 Oktoba 2006
Waigizaji wageni
Wendo wa sehemu
← Iliyopita Ijayo →
"Genesis" "One Giant Leap"
Orodha ya sehemu za Heroes

"Don't Look Back" ni sehemu ya pili ya msimu wa kwanza wa igizo la ubunifu wa kisayansi linalorushwa hewani na kituo cha televisheni cha NBC, Heroes. Sehemu imeongozwa na Allan Arkush na kutungwa na Tim Kring. Sehemu hii wahusika wanapambana na matokeo ya matendo yao kwenye "Genesis". Peter amepona baada ya kuanguka kwake, Hiro anapeleleza mjini New York, Niki anahangaika na matokeo ya mauaji aliyoyafanya, na Mohinder bado anaendelea na uchunguzi wa kifo cha baba yake.

Hadithi (kwa ufupi)[hariri | hariri chanzo]

Peter ana amka akiwa hospitalini baada ya shemu iliyopita, ambapo Nathan anakataa katakata kwamba walipaa. Mama yao anagundua kwamba baba yao alikuwa akisumbuliwa na mfadhaiko, na kuhisi kwamba Peter alikuwa akisumbuliwa na mfululizo wa madanganyo ambayo yanamfanya ajione kwamba haonekani, lakini imempelekea huku kuanguka kwake. Peter akawa na huzuni sana baada ya kuona kwamba hakuna anayemwamini na yale asemayo, na baadaye akaenda kusimama juu kabisa ya kilele cha jengo la New York City. Kwa bahari nzuri, Nathan amemkuta kwa muda mwafaka, ijapokuwa Peter anamwamuru kaka yake amwambie ukweli, na akakubali kama kweli alipaa. Wkati anasema haya, inagundulika kama anavinjari juu ya anga.

Rafiki wa Claire, Jackie, anachukua ujiko wa kijitia yeye ndiye aliyemwokoa mtu katika moto kwenye sehemu iliyopita, na Zack anagundua kwamba hazioni zile video za Claire anazojiumiza mwenyewe. Baadaye, Mr. Bennet akasadiki ya kwamba Claire amekua vya kutosha, na kumweleza kwamba anafanya mpango wa kumkutanisha na wazazi wake halisi. Bila Claire kujua, Mr. Bennet kazipata zile video zake.

Mohinder amekutana na Eden McCain, rafiki wa baba yake ambaye anaamini nadharia zake. Mtu mmoja aitwaye Sylar anajaribu kuwasiliana na Chandra, anagundua "ana njaa" hajiwezi tena. Mohinder na Eden wameokota flash drive ambayo ina programu ambayo Chandra aliitumia kwa ajili ya utafiti wake. Penginepo, katika eneo la mauaji, afisa wa Matt Parkman anasikia sauti ya msichana mdogo kwenye kichwa chake. Anafuatilia, na kumkuta binti wa wahanga amejificha. Pia amewasikia kwa mbali wapelelezi wakitaja kwamba mtuhumiwa anaitwa Sylar. Kachero wa FBI Audrey Hanson anauliza maswali Matt amejuaje sehemu ambayo yule msicha amejificha, na matokeo yake wakamweka chini ya ulinzi kwa kumwekea mashaka ya kushiriki kwenye mauaji hayo.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]