Micah Sanders

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Micah Sanders
muhusika wa Heroes

Noah Gray-Cabey kama Micah Sanders
Mwonekano wa kwanza "Genesis"
Mwonekano wa mwisho "I Am Sylar"
Imechezwa na Noah Gray-Cabey
Maelezo
Majina mengine Mwasi
UwezoTechnopathy

Micah Sanders, imechezwa na Noah Gray-Cabey, ni jina la kutaja muhusika wa kipindi cha mfululizo wa maigizo ya ubunifu wa kisayansi cha kwenye televisheni ya NBC, Heroes. Huyu ni mtoto wa Niki Sanders na D.L. Hawkins. Yeye ni mtoto mwenye kipaji cha hali ya juu na vilevile ni technopath (kwa maana ya kimtathilia humaanisha mtu mwenye uwezo wa kuchezea teknolojia kwa jinsi vile apendavyo).

Mwanzo[hariri | hariri chanzo]

Miezi sita ya awali, mwanzoni kabisa mwa mfululizo, Micah anapata laptop mpya kutoka kwa babu yake, Hal, ambaye amefarakana na familia yake. Wakati Hal anagundua kwamba Micah anaichengua ile laptop, babu kapandisha jazba, lakini kwa bahati Niki kwanza alishampiga topu aondoke nyumbani kwao, na kisha baadaye kumfuatilia kidogo-kidogo akiwa kama Jessica na kumtandika, akimwamuru kwamba aachane kabisa na maisha yake na ya Micah.

Micah ameonekana kwa mara ya kwanza katika "Genesis" wakati anakarabati motherboard ya kwenye kompyuta yake wakati Niki anakuja kumtazama. Wamekutwa na makachero wa Linderman na wanajipanga kukimbia huku Niki anamwona mtu kwenye kioo ambaye si yeye. Micah ameondoka na shoga wa Niki "Texas" Tina.

Kwenye "Don't Look Back", Niki anamchukua Micah na kwenda naye jangwani, kwa kufuata ramani ya ajabu ambayo ameikuta ndani ya buti la gari ambalo lina miili iliyopondeka.

Kufuatia mgogoro baina ya Niki na mama-mkwe-wake kwenye kipengele cha "One Giant Leap", Niki na Micah wanachukuliwa na washirika wa Linderman.

Micah anagundua kazi ya Niki akiwa kama mjiambuaji wa webcam kwenye "Collision", na kuonelea kwamba kazi yake ni "salama kwenye Internet" kuliko kuifanyia ugani, inaonekana dhajiri kwamba Niki anapanga kulala na Nathan ili kumwokoa Micah.

D.L. Hawkins anarudi kwenye kipengele cha "Better Halves" kufanya marekebisho na familia yake ili aondoke nayo. Hata hivyo, baada ya Micah kutoa siri ya Niki kwake, ana-tuhumu kwamba Niki si yeye wakati Jessica anashika hatamu, na ugomvi umefichua kila wakati D.L. anamchukua Micah kutoka mikononi mwa Niki.