Nothing to Hide

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
"Nothing to Hide"
Sehemu ya Heroes
Heroes s01 e07.jpg
Micah anagundulika kama kuwa ni teknopathi.
Sehemu ya. Msimu 1
Sehemu 7
Imetungwa na Jesse Alexander
Imeongozwa na Donna Deitch
Tayarisho la 107
Tarehe halisi ya kurushwa 6 Novemba 2006
Waigizaji wageni
Wendo wa sehemu
← Iliyopita Ijayo →
"Better Halves" "Seven Minutes to Midnight"
Orodha ya sehemu za Heroes

"Nothing to Hide" ni sehemu ya saba ya msimu wa kwanza wa mfululizo wa igizo la ubunifu wa kisayansi linalorushwa hewani na kituo cha televisheni cha NBC, Heroes.

Hadithi[hariri | hariri chanzo]

Peter[hariri | hariri chanzo]

Peter anasoma taarifa ya soko la hisa kwa bwana Charles Deveaux. Baada ya mazungumzo juu ya taarifa hiyo, Peter na Charles wanasema "Tupendane", yaonesha ukaribu mno,yaani, kama mahusiano ya baba na mwana. Baada ya muda Charles akaanza kuhoa. Baada ya kumkagua, Peter anagundua kama anaweza kupaa, lakini Charles hamwamini. Peter kisha anaonekana akielekea kwenye dirisha lililokuwa wazi na kuanza kupaa huku kamera ikionesha mfano wa kitu kinachopaa kwenye majengo marefu. Kengere ya mlango inamwamsha Peter, na kugundua kwamba kipande kilichopita ilikuwa ni ndoto. Anafungua mlango na kumkuta Simone Deveaux nje analia. Ana mtaarifu kwamba baba yake amefariki saa limoja lililopita. Peter na Simone wanaenda kumuona Isaac nyumbani kwake, walichokuta na kwamba kumevurugwa na Isaac hayupo. Simone anaeleza kwamba baba yake alizungumzia amepaa dunia nzima na Peter na hivyo ameona vitu vibaya vingi, japokuwa Peter amemwakikishia kwamba kila kitu kitakuwa sawa hivyo basi asiie shaka, anamwambia kulikuwa kuna watu wanajali, na walikuwa na mpango wa kuisadia dunia. Peter anajibu kwamba hajawahi kufanya mazungumzo ya namna hiyo na baba yake Simone. Simone anamwambia Peter kwamba picha ambayo yeye na Isaac walikuwa wakiitafuta imeuzwa kwa "Linderman".

Nathan[hariri | hariri chanzo]

Nathan na mkewe, Heidi, wanang'amu namna gani watashinda kwenye uchaguzi mkuu wa rais. Mama wa Nathan ameratibu mahojiano na gazeti kubwa nchini ilimradi afanye utambulisho wa familia kwa watu wa nje, tabia ambayo awali familia haikuwa nayo. Nathan na Heidi wanajadili namna ya yeye kuonekana mbele ya kadamnasi, wakati alikuwa hayupo wakati wa kampeni zake, na anaeleza ya kwamba ana hamu ya hilo. Heidi, tunagundua, matumizi ya kiti cha magurudumu ni matokeo ya ajali ambayo Nathan ana husika nayo. Oliver Dennison anagundua kwamba Heidi yupo sawa tu kwenye kiti cha magurudumu. Anasema kwamba alikuwa na na hasira kwa muda mrefu sana, lakini hayo ni ya Mungu - na si Nathan, kama jinsi Mr Dennison alivyoonelea - kwa yule ambaye hasira zake alizielekezea. Peter anawasili kwenye utambulisho na kutoa maoni ya ukweli kwamba familia haina utaratibu huo wa kutambulisha wageni wa nje familia yao. Nathan amemtoa nje kidogo na kujibu kwamba Peter hajakuwa na kufahamu umuhimu wa utambulisho, ikiwa uwepo wake utaharibu uchaguzi wake. Peter anamwomba Nathan amsaidie kuirudisha ule mchoro ambao Linderman ameununua kutoka kwa Simone, lakini Nathan kakataa. Peter kisha anamtishia Nathan kwamba atatoa siri yake kama ana uwezo wa kupaa kwa Mr Dennison, anamwacha Nathan kutokuwa na jinsi. Kwenye katafrija kale, Mr. Dennison anamhabrisha Nathan kwamba mshirika wake wa zamani wa wa ulinzi ametoa taarifa kwamba kulikuwa na vitisho mjini Las Vegas kuhusu umepotevu wake, na kuongezea kwamba vitisho hivyo kuna mshirikisha mwanamama mmoja mwenye nywele za manjano. Peter haraka akamtetea kaka yake na kudai kwamba Nathan aliongea na mwanamke mmoja ambaye ni daktari wa kliniki ambayo ipo nje kidogo ya mji wa Las Vegas kwa ajili ya matiabu ya matatizo ya akili ya Peter.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]