Truth & Consequences

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
"Truth & Consequences"
Sehemu ya Heroes
Heroes Truth & Consequences.jpg
Claire akimpiga mkwara Elle.
Sehemu ya. Msimu 2
Sehemu 10
Imetungwa na Jesse Alexander
Imeongozwa na Adam Kane
Tayarisho la 210
Tarehe halisi ya kurushwa November 26, 2007
Waigizaji wageni
Wendo wa sehemu
← Iliyopita Ijayo →
"Cautionary Tales" "Powerless"
Orodha ya sehemu za Heroes

"Truth & Consequences" ni sehemu ya kumi ya msimu wa pili wa tamthilia ya ubunifu wa kisayansi inayorushwa hewani na TV ya NBC - Heroes. Ilianza kurushwa kuanzia tar. 26 Novemba, 2007.[1] Katika kurushwa kwake kwa mara ya kwanza, ilipokea watazamaji milioni 11.89.[2]

Hadithi[hariri | hariri chanzo]

Peter Petrelli na Adam Monroe wanamsaka Victoria Pratt (Joanna Cassidy) huko mjini Searsmont, Maine, ili kujua wapi walificha Shanti virus. Pale alipoona Peter yupo pamoja na Adam, anapiga risasi kwa wote wawili huku akijiandaa kumuangamiza Adam moja kwa moja, hadi Peter alivyomzimisha. Alipopata fahamu, Peter anasoma mawazo ya Vicky na kugundua kirusi cha Shanti kimetunzwa huko mjini Odessa, Texas. Pratt anajaribu kumtandika risasi Peter, lakini Adam anapandisha mzuka na kumuua Pratt.

Claire Bennet na familia yake wanatembelewa na Bob, ambaye anawapa kile anachodai ni majivu ya Noah Bennet. Bob anampa kazi binti yake, Elle, ya kumwangalia Claire. Claire anamzingua Elle na kutishia kupuliza firimbi ya kutoa ukweli mbele ya hadhara juu ya kina Company.

Bob na Mohinder Suresh wanarumbana juu ya matumizi ya damu ya Claire ili kumfufua Noah. Damu ya Claire imeisadia damu ya Mohinder kutengeneza tiba ya kirusi tena. Mohinder kisha anamsisitizia Bob ya kwamba wasaidiane kuangamiza vyanzo vyote vya utengenezaji wa virusi hivyo.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Cite error: Invalid <ref> tag; no text was provided for refs named ep
  2. Weekly Program Rankings (Press release). ABC Medianet. December 4, 2007. Archived from the original on 2008-06-18. https://web.archive.org/web/20080618031639/http://www.abcmedianet.com/Web/progcal/dispDNR.aspx?id=120407_05. Retrieved 2007-12-19.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]