Nenda kwa yaliyomo

Heroes

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Heroes (TV series))
Heroes

Nembo ya Heroes
Aina Maigizo
Aksheni
Shujaa mkuu
Nchi inayotoka Marekani
Lugha Kiingereza
Ina misimu 4
Ina sehemu Los Angeles, California
Utayarishaji
Watayarishaji
wakuu
Tim Kring
Dennis Hammer
Allan Arkush
Greg Beeman
Adam Armus
Kay Foster
Jim Chory
Jesse Alexander
Michael Green
Jeph Loeb
J.J. Philbin
Aron Eli Coleite
Mhariri {{{Mhariri}}}
Sehemu Los Angeles, California
Muda makisio ni dk. 43
Urushaji wa matangazo
Kituo NBC
Inarushwa na 25 Septemba 2006 - hadi leo
Viungo vya nje


Heroes ni kipindi cha Marekani kilichobuniwa na Tim Kring, kwenye stesheni ya NBC mnamo 25 Septemba 2006. Kipindi hiki kinaeleza jinsi wahusika wanajitambua kama wana vipawa mbalimbali na jinsi vipawa hivi vinavyoathiri maisha yao.

Misimu tatu imeshaonyeshwa na ya nne ilianza mnamo 21 Septemba 2009. Msimu wa kwanza ulivutia watazamaji milioni 14.3 nchini Marekani. Msimu wa pili wa Heroes ilivutia watazamaji milioni 13.1 nchini Marekani.[1]

Msimu wa kwanza

[hariri | hariri chanzo]
Picha ambayo Isaac alichora

Msimu wa kwanza ina vipindi 23 ambavyo vilionyeshwa kuanzia 25 Septemba 2006 hadi 21 Mei 2007.[2] Inatuonyesha jinsi kundi la binadamu wanavyotambua kuwa wana vipawa fulani. Mohinder Suresh, ambaye ni daktari na profesa, anafanya utafiti kuhusu watu hawa wenye vipawa. Wote wanajaribu kukabiliana na vipawa waliyonayo, wakijaribu kila mbinu kuzuia mlipuko wa bomu utakaotokea mjini New York City.

Msimu wa pili

[hariri | hariri chanzo]

Ilianza 24 Septemba 2007. Ina jumla ya vipindi 11. Watu hawa wenye vipawa ("heroes") wanashirikiana na kuja pamoja ili kuzuia uenezaji wa virusi utakaouwa watu wote duniani.

Msimu wa tatu

[hariri | hariri chanzo]

Ina vipindi 25 iliyoanza kuonyesha mnamo 22 Septemba 2008.[3] Inaanza pindi Nathan Petrelli karibu auwawe. Wafungwa wanapata nafasi ya kukimbia jela na "The Company" inawasaka. Pia, wanatafuta namna ya kuwafanya binadamu wa kawaida wapate vipawa.Sylar anatafuta wazazi wake wa ukweli. Mwishowe, Nathan anauliwa baada ya kupigana na Sylar. Matt anamsakanya Sylar ili asiwe na uwezo wa kuwanasa watu wenye vipawa.

Msimu wa nne

[hariri | hariri chanzo]

Mnamo 4 Mei 2009, NBC walitangaza kuwa Heroes msimu wa nne itakuwa na vipindi 19.

Wahusika Wakuu

[hariri | hariri chanzo]

Mafanikio

[hariri | hariri chanzo]
Msimu Saa Mwanzo wa msimu Mwisho wa msimu Mwaka Watazamaji
milioni
Watazamaji + DVR Watazamaji (BBC2)
1 Monday 9:00 pm 25 Septemba 2006 21 Mei 2007 2006–2007 13.86 14.30 3.91
2 Monday 9:00 pm 24 Septemba 2007 3 Desemba 2007 2007–2008 11.46 13.10 3.81
3 Monday 9:00 pm 22 Septemba 2008 27 Aprili 2009 2008–2009 7.61 9.27 3.26
4 Monday 8:00 pm (2009)
Monday 9:00 pm (2010)
21 Septemba 2009 - 2009–2010 5.36^ - -
  1. "NBC Renews Drama Series Chuck, Life and Heroes for 2008-09 Season". 2008-02-13. Iliwekwa mnamo 2008-02-13.
  2. "Heroes: How to Stop an Exploding Man - TV.com". TV.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2010-03-30. Iliwekwa mnamo 2008-04-19.
  3. Adalian, Josef (2008-05-23). "NBC Revamps Fall Plans, Delays Series Launches". TVWeek.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2010-02-12. Iliwekwa mnamo 2008-09-18.