Ali Larter

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ali Larter

Larter at the 64th Annual Golden Globe Awards.
Amezaliwa Alison Elizabeth Larter
28 Februari 1976 (1976-02-28) (umri 48)
Cherry Hill, New Jersey, U.S.
Jina lingine Allegra Coleman[1]
Kazi yake Mwigizaji
Miaka ya kazi 1997–hadi sasa
Ndoa Hayes MacArthur (2009–hadi sasa)

Alison Elizabeth "Ali" Larter (amezaliwa tar. 28 Februari 1976) ni mwigizaji wa fiamu na mwanamitindo wa zamani kutoka nchini Marekani. Ameanza kazi za uigizaji ni baada ya kuonekana kidogokidogo kwenye vipipindi kadhaa vya televisheni kunako miaka ya 1990. Kuanzia 2006 hadi 2010, Larter amecheza nyusika za Niki Sanders halafu ndugu wa kashinde wake-waliopoteana muda mrefu Tracy Strauss kwenye mfululizo wa TV wa ubunifu wa kisayansi wa kwenye NBC, Heroes.[2][3]

Larter ameanza kazi kama mwanamitindo lakini baada ya muda mfupi akajiingiza kwenye masuala ya uigizaji. Ameanza kujipatia umaarufu wa hali ya juu baada ya kushiriki kwenye filamu ya mwaka wa 1999, Varsity Blues. Hii ilifuatiwa na filamu ya kutisha ya House on Haunted Hill (1999), Final Destination (2000), na Legally Blonde (2001). Tangu hapo, akaanza kucheza kwenye nyusika za juu tena ikiwa ni pamoja na kurudia uhusika wake kwenye Final Destination 2 (2003), amecheza kama muhusika wa jina tu kwenye filamu ya Bollywood ya Marigold (2007) na kucheza kama muhusika wa mchezo wa video Claire Redfield kwenye Resident Evil: Extinction. Hivi karibuni, amecheza kwenye picha ya kusisimua ya mwaka wa 2009, Obsessed.

Larter amepewa jina kwenye orodha ya "Wanawake Wazuri Walio-Hai".[4] Ameolewa na bwana wake aliyedumu naye kwa muda wa miaka mitatu, Hayes MacArthur, kwa sherehe ndogo tu huko mjini Maine mnamo tar. 1 Agosti 2009.[5]

Maisha ya wali na Uanamitindo[hariri | hariri chanzo]

Larter alizaliwa mjini Cherry Hill, New Jersey. Ana ndugu yake wa kike mkubwa aitwaye Kirsten, ambaye ni mwalimu. Yeye ni binti wa Bi. Margaret, mama wa nyumbani, na Danforth Larter, mkurugenzi wa usafiri w magari makubwa.[6][7] Alihitimu katika shule ya Carusi Middle School na Cherry Hill High School West. Larter ameanza kazi zake za uanamitindo akiwa na umri wa 14 wakati skauti wa uanamitindo amegundua kipaji chake mtaani kwao. Ameombwa kushiriki kwenye matangazo ya biashara ya Phillies na baadaye kutia saini mkataba wa kiuanamitindo na Ford Modeling Agency mjini New York. Larter baadaye karuka mwaka wake mkuu na kwenda kufanya uanamitindo nchini Japan na Australia. Akiwa na umri wa miaka 17, Larter akatulia kidogo nchini Japan.[8] Baadaye, mnamo 1995, kamsindikiza bwana'ke katika safari yake ya kuhamia mjini Los Angeles, California.

Filmografia[hariri | hariri chanzo]

Mwaka Filamu Uhusika Maelezo
1999 House on Haunted Hill Sara Wolfe
Varsity Blues Darcy Sears
Drive Me Crazy Dulcie
Giving It Up Amber aka Casanova Falling
2000 Final Destination Clear Rivers Young Hollywood Award for Breakthrough Performance Female
Nominated — Blockbuster Entertainment Award — Favorite Actress - Horror
2001 American Outlaws Zerelda 'Zee' Mimms
Jay and Silent Bob Strike Back Chrissy
Legally Blonde Brooke Taylor Windham
2003 Final Destination 2 Clear Rivers
2004 Three Way Isobel Delano aka 3-Way
Pia Mtayarishaji Msaidizi
2005 Confess Olivia Averill
A Lot Like Love Gina
2007 Marigold Marigold Lexton Bollywood
Resident Evil: Extinction Claire Redfield
Homo Erectus Fardart aka National Lampoon's The Stoned Age
2008 Crazy Evelyn Garland
2009 Obsessed Lisa Sheridan MTV Movie Award — Best Fight (amepeana na Beyoncé Knowles)
Amechaguliwa — Teen Choice Award — Choice Movie Rumble (amepeana na Beyoncé Knowles)
Amechaguliw — Golden Raspberry Award — Worst Supporting Actress
2010 Resident Evil: Afterlife Claire Redfield (inasubiri kutolewa)

Televisheni[hariri | hariri chanzo]

Mwaka Kipindi Uhusika Maelezo
1997 Suddenly Susan Maddie Sehemu: "The Ways and Means"
Chicago Sons Angela Sehemu: "Beauty and the Butt"
1998 Chicago Hope Samantha Sehemu: "Memento Mori"
Just Shoot Me! Karey Burke Sehemu: "College or Collagen"
Dawson's Creek Kristy Livingstone Sehemu: "The Dance" and "The Kiss"
2004 Entourage Ali Larter Sehemu: "Pilot"
2006–2010 Heroes Niki / Jessica Sanders / Tracy Strauss Gracie Allen Awards — Outstanding Supporting Actress — Drama Series
Teen Choice Award — Choice TV Actress: Action Adventure
Nominated — Saturn Award for Best Supporting Actress on Television
Nominated — Scream Award — Sexiest Superhero
Nominated — SyFy Genre Awards — Best Supporting Actress/Television
Nominated — Teen Choice Award — Choice TV Actress: Action Adventure

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Biography for Ali Larter. IMBd. Iliwekwa mnamo 2010-06-27.
  2. Heroes Cast Members, Tracy Strauss. NBC. Iliwekwa mnamo 2010-07-24.
  3. Feinburg, Daniel. "NBC's 'Heroes' Fascinates Larter", Zap2it, 2006-07-03. Retrieved on 2010-06-27. Archived from the original on 2012-09-26. 
  4. Ali Larter. Celebritywonder.com. Iliwekwa mnamo 2010-02-30.
  5. Everett, Christina. "'Heroes' star Ali Larter marries actor Hayes MacArthur in Maine", New York Daily, 2009-08-03. Retrieved on 2010-06-27. Archived from the original on 2009-09-07. 
  6. Ali Larter Biography. Tvguide.com. Iliwekwa mnamo 2007-08-27.
  7. Fahner, Molly. "Fun Fearless Female of the Year: Ali Larter", Cosmopolitan. Retrieved on 2010-06-27. 
  8. Ali Larter Biography. Yahoo.com. Iliwekwa mnamo 2007-08-27.

Soma zaidi[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]