Tracy Strauss

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Tracy Strauss
muhusika wa Heroes
Mwonekano wa kwanza "The Second Coming"
Mwonekano wa mwisho "Brave New World"
Sababu Mwisho wa mfululizo
Maelezo
Kazi yake Mshauri wa Kisiasa
UwezoKugandisha
Kujibadilisha kuwa maji

Tracy Strauss, umechezwa na Ali Larter, ni jina la kutaja mhusika wa kipindi maarufu cha ubunifu wa kisayansi kinachorushwa hewani na televisheni ya NBC, Heroes. Ana uwezo wa kugandisha kitu chochote anachogusa. Kadiri mfululizo unavyoendelea, uwezo wake unakua hadi kufikia kiasi cha kujigeuza hata kuwa maji. Alianza kuonekana kwenye msimu wa tatu, yeye ni mshauri mkuu wa gavana wa New York ambaye ndiye aliyemvuta Nathan Petrelli awe seneta.

Huyu ni dada kashinde wa Niki Sanders na Barbara, wote walibadilishwa vinasaba vyao na Dr. Zimmerman na kutengenezwa kiuzazi. Pia ni mama mdogo wa kuzaliwa na Micah Sanders. Kulingana na watunzi Joe Pokaski na Aron Coleite, Niki aliondolewa kwenye mfululizo na badala yake akawekwa Tracy hivyo basi Larter ataweza kucheza uhusika tofauti-tofauti, pindi walipogundua ya kwamba hawatoendelea zaidi na uhusika huo.

Mabadiliko hao nayo yamewawezesha kuelezea chimbuko la hadithi yao, ambapo mhusika anagundua kuwa ana vipawa.[1]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Pokaski, Joe; Coliete, Aron (6 Oktoba 2008). "Behind the Eclipse: Week 2". Comic Book Resources. Iliwekwa mnamo 2008-11-04.  Check date values in: |date= (help)