Noah Gray-Cabey

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Noah Gray-Cabey

Noah Gray-Cabey, Aprili 2009
Amezaliwa 16 Novemba 1995 (1995-11-16) (umri 28)
Chicago, Illinois, US
Kazi yake Actor
Pianist
Miaka ya kazi 2002–present

Noah Gray-Cabey (amezaliwa 16 Novemba 1995) ni mwigizaji wa filamu na televisheni na mpigaji piano wa kutoka Marekani. Alipata umaarufu wa kuigiza kwenye kipindi cha kuchekesha cha My Wife and Kids kama Franklin Aloysius Mumford na Micah Sanders katika kipindi cha sayansi kiitwacho Heroes inayoonyeshwa kwenye stesheni ya NBC.

Maisha ya awali[hariri | hariri chanzo]

Gray-Cabey alizaliwa tarehe 16 Novemba 1995 mjini Chicago, Illinois. Wazazi wake ni Whitney Gray na Shawn Cabey. Aidha alikulia maisha yake mjini Newry, Maine. Alianza kucheza na kidude che piano. Yeye amedai katika mahojiano kuwa wakati alipofikia umri wa miaka minne, aliamua kwamba alitaka kucheza piano halisi. Alipokuwa na miaka minne, alichezesha piano katika kumbi kadhaa nchini Uingereza na Washington, na alisafiri hadi Jamaika kwa ziara yake ya kwanza pamoja na New England Symphonic Ensemble. Julai 2001, Nuoah aliendelea kuzuru Australia, na alipokuwa na umri wa miaka mitano, yeye alikuwa mtu wa kwanza mwenye umri mdogo zaidi kupiga piano pamoja na "orchestra" katika Jumba la Sydney Opera, Queensland Conservatory na hata Mkataba wa Kimataifa mjini Brisbane. Yeye alionyeshwa kwenye Ripley's Believe It or Not kwa ajili ya talanta yake.[1]

Kazi[hariri | hariri chanzo]

Filamu na televisheni[hariri | hariri chanzo]

Gray-Cabey alianza kuigiza kwenye filamu ya Lady in the Water kama "Joey Dury". Alianza kuigiza mnamo Desemba 2001 na amewahi kuonekana kwenye My Wife & Kids akiigiza nafasi ya Franklyn Aloysius Mumford, 48 Hours, Grey's Anatomy, The Tonight Show, Good Morning America na Oprah Winfrey Show. Sasa yuko kwenye kipindi kinachovuma cha Heroes akiigiza kama mwana wa Niki Sanders na DL Hawkins. Kwenye hiki kipindi, aliigiza kama mtu mwenye kipawa cha kuamrisha mashine.

AIM - Action in Music[hariri | hariri chanzo]

AIM ni mradi ulioanzishwa na wazazi wa Gray-Cabey. Madhumuni ya AIM ni kuwasaidia watoto kuendeleza vipaji vyao vya muziki na kuwapa fursa ya kutumbuiza katika nchi nyingine. Pesa zinazotoka kwa matamasha haya hupelekwa kwa hospitali na nyumba za mayatima katika nchi hizo.[2] Amewahi kurekodi CD akiwa na familia yake, wakiimba vipande vya Bach, Haydn na Vivaldi na nyingineyo. CD hii pia inaonyesha Noah akipiga paino alipokuwa na umri wa miaka 5.[3]

Maisha ya Kibinafsi[hariri | hariri chanzo]

Gray-Cabey anapenda kucheza michezo ya video na kuangalia filamu. Alipoulizwa kuwa angependa kupewa kipawa kipi katika maisha halisi, yeye alijibu, "Ningependa labda kuwa uwezo wa kuzungumza na wanyama kwa sababu napenda kufuga wanyama; mimi nafuga mbwa na paka." Yeye anahudhuria Shule ya Upili ya Paraclete.[4]

Filamu[hariri | hariri chanzo]

mwaka Filamu Dhima Vidokezo
2002 My Wife and Kids Franklin Aloysius Mumford vipindi 60; 2002-2005
2003 Ripley's Believe it or Not mwenyewe kipindi 1
2004 CSI: Miami Stevie Valdez Kipindi: "Pro Per"
2006 Grey's Anatomy Shawn Beglight Kipindi: "What Have I Done kwa Deserve This?"
Ghost Whisperer Jameel Fisher Kipindi: "Fury"
Lady in the Water Sam Dury
Heroes Mika Sanders 2006-2007-2008
2010 CSI: Crime Scene Investigation Steve Reppling

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. [http:// IMDb - Noah Grey-Cabey]. Iliwekwa mnamo 2007-09-19.
  2. A.I.M. Gray, Whitney. Jalada kutoka ya awali juu ya 2007-08-25. Iliwekwa mnamo 2007-09-19.
  3. A.I.M. Store. Jalada kutoka ya awali juu ya 2007-08-23. Iliwekwa mnamo 2007-09-03.
  4. Nakala iliyohifadhiwa. Jalada kutoka ya awali juu ya 2009-04-12. Iliwekwa mnamo 2021-02-17.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu mwigizaji filamu fulani wa Marekani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Noah Gray-Cabey kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.