One Giant Leap
"One Giant Leap" | |||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|
Sehemu ya Heroes | |||||||
Mohinder Suresh anagundua maswali zaidi. | |||||||
Sehemu ya. | Msimu 1 Sehemu 3 | ||||||
Imetungwa na | Jeph Loeb | ||||||
Imeongozwa na | Greg Beeman | ||||||
Tayarisho la | 103 | ||||||
Tarehe halisi ya kurushwa | 9 Oktoba 2006 | ||||||
Waigizaji wageni | |||||||
| |||||||
Orodha ya sehemu za Heroes |
"One Giant Leap" ni sehemu ya tatu ya msimu wa kwanza wa mfululizo wa kipindi cha televisheni cha ubunifu wa kisayansi - kinachorushwa hewani na kituo cha NBC, Heroes. Imeongozwa na Greg Beeman na kutungwa na Jeph Loeb.[1]
Hadithi
[hariri | hariri chanzo]Niki anamalizia kuzika majambazi waliokufa kwenye sehemu iliyopita. Baada ya hapo, kaenda kulumbana na mama-mkwe-wake, ambaye anaamini kwamba Niki hawezi kumtunza Micah. Pia amegundua ya kwamba D.L. ametoroka jela. Baadaye, Niki na Micah wakachukuliwa kwa kutaka na mmoja kati ya watu wa Mr. Linderman.
Baada ya ushindi wa timu ya shule anayosoma, Claire anahudhuria ushindi wa timu. Brody Mitchum, kiungo wa timu, anaongea na Claire na kumchukua nje kidogo ya kundi, na kujaribu kumbaka. Baada ya jitahada chache, kichwa cha Claire kikachoma kwenye kijitawi cha mti. Mwishoni mwa sehemu, uchunguzi wa mwili uliokuwa ukifanywa kwa Claire, na mara baada ya kile kitawi kutolewa, inasababisha kufufuka kwake.
Hiro anarudi katika masaa ya kawaida, ambapo anamwonesha Ando kitabu cha picha ambacho kinaonesha maneno na vitendo vilevile anavyoongea yeye na Ando. Hiro anamshawishi Ando amfuate Marekani, ambapo watakuwa na jukumu la kuokoa dunia dhidi ya janga la mlipuko wa bomu ambalo Hiro amelishuhudia alipoenda baadaye.
Peter bado ana hasira na Nathan kwa kukana hali halisi walizonazo; Nathan ana wasiwasi sana na mwonekano wa Peter kwenye vyombo vya habari. Kwenye sherehe za kampeni jioni moja, Nathan anadai ya kwa wageni wake kwamba Peter alikuwa na mfadhaiko, na akajaribu kujiua. Kwa hilo Peter lilimkera na kuamua kuondoka, kwa hasira, lakini kakutana na Simone, ambaye alikiri kwamba anampenda wakati fulani uliopita, basi wakabusiana.
Mohinder na Eden wamepata anwani ambayo inaonesha kuwa makazi ya Sylar. Huko, wamekuta ya kwamba Sylar ana habari nyingi juu ya wapi pa kuwapata wahusika wenye nguvu za ajabu, vilevile jumbe za kukiri makosa kutoka kwa Sylar. Baadaye, wakarudi na kukuta kila shaghalabaghala.
Matt anamshawishi Audrey kwamba yeye hana hatia na anaweza kusoma fikra za mtu. Audrey anampatia kazi na FBI. Sylar anafanikiwa kumpata Molly na kujaribu kumwua, lakini alishambuliwa na Matt na Audrey. Licha ya kupata majelaha kadha wa kadha ya silaha, aliweza kuinuka na kutoroka. Nyumbani, Matt na mkewe wanazozana, na Matt anaondoka. Kwenye baa, anamwona mtu asiyejulikana ambaye fikra zake hawezi kuzisoma, na matokeo yake Matt anaanguka na kupoteza fahamu.
Isaac anamlazimisha Simone aondoke pale aliposema aamini tabiri zake. Baadaye, Isaac anaona michoro aliyochora watu wawili wanapigana kwenye mvua — Simone na Peter.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]Viungo vya Nje
[hariri | hariri chanzo]- Watch "One Giant Leap" at NBC.com
- One Giant Leap at the Internet Movie Database
- Beaming Beeman: Episode 3: One Giant Leap Director's blog on the filming of this episode.