Nenda kwa yaliyomo

Elle Bishop

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Elle Bishop
muhusika wa Heroes
Elle Bishop Heroes.jpg
Kristen Bell kama Elle Bishop
Mwonekano wa kwanza "Fight or Flight"
Mwonekano wa mwisho "The Eclipse: Part 2" (Elle wa ukweli)
"The Art of Deception" (kwenye kumbukumbu ya Sylar)
Imechezwa na Kristen Bell
Maelezo
Kazi yake Kachero wa kina Company
UwezoElectric manipulation
Jina kamiliEleanor Zoe Bishop

Eleanor Zoe Bishop, hujulikana zaidi kama Elle, ni jina la kutaja uhusika wa tamthilia kwenye kituo cha TV cha NBC, Heroes. Uhusika umechewa na Kristen Bell. Elle alianza kuonekana akiwa kama muhusika mpya kwenye Msimu wa Pili kwa mujibu wa mkataba, ameendelea kuwepo kwenye mfululizo angalau kwa sehemu takriban 13 katika Msimu wa Tatu.

Elle ameanza kutambulishwa katika sehemu ya "Fight or Flight" akiwa kama kachero wa kina Company, shirika ambalo msingi wake hasa ni kuwatambulisha, kuwaongoza na kuwasoma hao watu wenye vipawa mahususi. Yeye ni binti wa mkuu wa Company bwana Bob Bishop, anamiliki kipawa na kuzalisha na kuchezea umeme. Elle amecheza kama ana-matatizo ya kiakili kwa namna fulani, kitendo ambacho kilipelekea baba'ke ajaribu tafiti zake kwa mwanawe wakati yungali mdogo.