Maya Herrera

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Maya Herrera
muhusika wa Heroes

Dania Ramirez kama Maya Herrera
Mwonekano wa kwanza "Four Months Later..."
Mwonekano wa mwisho "The Eclipse, Part 2"
Imechezwa na Dania Ramirez
Maelezo
UwezoKumwaga sumu[1]
(nguvu zake zimeondolewa na Arthur Petrelli kwenye Msimu wa Tatu)

Maya Herrera ni jina la kutaja uhusika wa katika kipindi cha mfululizo wa televisheni wa ubunifu wa kisayansi ambao unarushwa hewani na kituo cha TV cha NBC, Heroes. Uhusika unachezwa na Dania Ramirez. Kuonekana kwake kwa mara ya kwanza katika sehemu ya "Four Months Later...", ingawa uhusika ulikuwepo tangu awali katika riwaya ya picha kama "Maya y Alejandro".

Muhtasari wa uhusika[hariri | hariri chanzo]

Generations[hariri | hariri chanzo]

Maya na pacha wake Alejandro ni watoro wanaotafutwa kwa kosa la mauaji. Kwenye "Four Months Ago...", inagundulika kama ameua watu wote waliohudhuria harusi ya kaka yake, kasoro Alejandro, na nguvu zake. Haya yametokea wakati Maya amegundua bibi harusi bado ana mahusiana ya kimapenzi na bwana wake wa zamani, na yule mwanaume akamtisha Maya, na kumsababishia mfadhaiko wa kutosha kuamsha nguvu zake.

Halafu baadaye kaamua kuwa mtawa na kwenda kuishi katika jumba la watawa huko nchini Venezuela na kumwomba Mungu amsaidiye matatizo yake. Hata hivyo, ndugu yake kampata na kumpeleka polisi. Tena amefedheheka katika harakati za kumfunga, nguvu zake zika-amka, lakini Alejandro, ametumia nguvu yake mwenyewe, na kuzuia uharibifu huo na kisha kutoroka.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]