Parasite (Heroes)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
"Parasite"
Sehemu ya Heroes
Heroes s01e18.jpg
Hiro na Ando wanatazama baadaye inayoangamia.
Sehemu ya. Msimu 1
Sehemu 18
Imetungwa na Christopher Zatta
Imeongozwa na Kevin Bray
Tayarisho la 118
Tarehe halisi ya kurushwa 4 Machi 2007
Waigizaji wageni
Wendo wa sehemu
← Iliyopita Ijayo →
"Company Man" ".07%"
Orodha ya sehemu za Heroes

"Parasite" ni sehemu ya kumi na nane ya msimu wa kwanza wa mfululizo wa kipindi cha ubunifu wa kisayansi kinachorushwa hewani na televisheni ya NBC, Heroes. Kipengele hiki kilikuwa maarufu kwamba, kwenye baadhi ya masoko, maneno ya utangulizi "Previously on Heroes" yaliandikwa kwa Kijapani na kuzungumzwa na Hiro, tofauti na yale ya Kiingereza ambayo daima hutumiwa.

Awali ilitangazwa kwa jina la "Like Any Parasite" hadi hapo NBC walipoamua kufupisha jina lake "Parasite" mnamo tar. 24 Februari 2007. Kama jinsi ilivyokuwa kwenye sehemu iliyopita, sehemu hii ilipata sifa sana kwenye masoko ya nchini Kanada kabla hata hao NBC hawajaitoa. Hii ilikuwa sehemu ya mwisho kurushwa hadi mnamo mwezi w Aprili 2007, pale mfululizo ulivyoibuliwa tena ili kumaliza msimu.

Hadithi[hariri | hariri chanzo]

Baada ya Simone Deveaux kufa, Isaac Mendez anamlaumu Peter Petrelli kwa kifo chake na kujaribu kumpiga risasi Peter, lakini Peter akajigeuza kutoonekana na kupaa kupitia dirishani. Akiwa kavurugwa, Peter anaenda kuomba msaada kwa Nathan. Nathan anasema kwamba atapiga simu polisi (bila kujulikana), ikiwaelekeza waende nyumbani kwa Isaac. Anamshauri Peter aende kupata msaada kutoka kwa Mohinder, lakini Peter akatoweka tena.

Thompson anamkandika maswali Mr. Bennet, ambaye anajielezea kwamba jambo la mwisho analokumbuka anamwendesha mkewe, Sandra, wakitokea hospitalini na kuelekea nyumbani. Hajui lolote kuhusu Claire wala the Haitian. Baadaye, nje ya chumba, Thompson na Candice Wilmer wanamchungua Bennet, akiwa pamoja na Matt Parkman, ambaye alishikiriwa kinyume na matakwa yake. Parkman anasema kwamba Mr. Bennet anaeleza ukweli.

Masaa machache baadaye, Mr. Bennet na Candice wanawasili nyumbani kwa Isaac. Candice amejigeuza kama Simone na kuficha maiti ya Simone ili kuwapumbaza mapolisi. Baadaye akajigeuza tena kuwa Simone ili kumfanyia mzaha Isaac, na kumwomba Mr. Bennet abaki. Lakini amekataa, anadai kwamba wametengeneza kisingizio, kinachosema Simone atakuwa Ulaya kwa muda usiojulikana.

Baada ya wale kuondoka, Isaac aliyevurugwa ameruadia tena matumizi yake ya heroini na kuchora picha kadhaa ambazo zinamtabiri yeye mwenyewe kichwa chake kimekatwa na ubongo umeondolewa, ikiwa sawa na wahanga wa Sylar.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]