Landslide (Heroes)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
"Landslide"
Sehemu ya Heroes
Heroes.S01E22 end.png
"Boom."
Sehemu ya. Msimu 1
Sehemu 22
Imetungwa na Jesse Alexander
Imeongozwa na Greg Beeman
Tayarisho la 122
Tarehe halisi ya kurushwa 14 Mei 2007
Waigizaji wageni
Wendo wa sehemu
← Iliyopita Ijayo →
"The Hard Part" "How to Stop an Exploding Man"
Orodha ya sehemu za Heroes

"Landslide" ni sehemu ya ishirini na mbili ya msimu wa kwanza wa mfululizo wa kipindi cha ubunifu wa kisayansi kinachorushwa hewani na televisheni ya NBC, Heroes. Ni sehemu ya pili ya vipande vitatu vya mwisho katika msimu wa kwanza.[1]

Hadithi[hariri | hariri chanzo]

Muungano wa Claire na Mr. Bennet umekatishwa ghafula na Peter ambaye amefikia hatua ya hatari ya kutojiweza baada ya kufyonza uwezo wa Ted. Peter anamwambia Claire ajiandae kwa kile anacholazimika kufanya ili kumzuia, lakini wakati Claire anajiandaa kutoa silaha kutoka katika mkoba wake, Peter ana nguvu ya kudhibi hali ya uwezo mpya na kujizuia mwenyewe asilipuke.

Akiwa mwenye huzuni, Hiro anasikitishwa ukosefu wa imani yake na upanga wake uliovunjika, Ando bado anaendelea kujaribu kurudisha nafsi ya Hiro. Ando anatafuta namba za simu kwenye Kurasa za Njano ili kukarabati upanga. Hiro anamzingua Ando kuhusu yule ambaye anamtarajia kumpa kwenye kitabu cha kumbukumbu ili kusawazisha mambo ya katana wa karne za kale, lakini Ando kafanikiwa kumpata mhunzi wa upanga akitangaza na nembo ya Helix.

Tukirudi mtaani, Mr. Bennet na Claire hatimaye wamepata nafasi ya kulonga. Mr. Bennet ameshangazwa kugundua uhusiano baina ya Peter na Claire na kumwelezea bintiye kuhusu mpango wake wa kuangamiza chombo cha ufuatiliaji na hivyo wataweza kuishi maisha yao ya kawaida tena; Claire anafikiria maisha ya kawaida haiwezekani, anatoa mazungumzo juu ya hali isiyo-ya-kawaida ya mpango wao, na kumweleza Bennet kwamba Peter huenda akawa na kitu cha "kuokoa dunia".

Wakati Peter anamshawishi Ted kwamba wawili hao wanastahili waondoke mjini New York City kabla hawajasababisha mlipuko, Mr. Bennet na[Matt Parkman|Parkman]] wanaendelea kutafuta chombo cha ufuatilizi. Claire, anaamini kwamba hii huenda ikawa ndiyo hatma yake, anaamua kuungana na Peter na Ted. Konani bila kutarajia mdukizi mwenye nguvu za kusikia majadiliano ya mbali: Sylar, ambaye ametambua mpango wa Peter wa kuondoka jijini, na kutazama nafasi ya kuendeleza zaidi mpango wake.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Lee, Patrick (2007-03-19). Heroes Finale Details Leaked. SciFi Wire. Iliwekwa mnamo 2007-03-19.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]