Homecoming (Heroes)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
"Homecoming"
Sehemu ya Heroes
Heroes s01 e09.jpg
Claire anamtazama Sylar akimshambulia Jackie, akiamini kuwa ni mkuu wa mashabiki mwenye nguvu za kipekee.
Sehemu ya. Msimu 1
Sehemu 9
Imetungwa na Adam Armus na Kay Foster
Imeongozwa na Greg Beeman
Tayarisho la 109
Tarehe halisi ya kurushwa 20 Novemba 2006
Waigizaji wageni
Wendo wa sehemu
← Iliyopita Ijayo →
"Seven Minutes to Midnight" "Six Months Ago"
Orodha ya sehemu za Heroes

"Homecoming" ni sehemu ya tisa ya msimu wa kwanza wa mfululizo wa igizo la ubunifu wa kisayansi linalorushwa hewani na kituo cha televisheni cha NBC, Heroes.

Hadithi[hariri | hariri chanzo]

Sehemu hii inaanza na Claire na rafiki yake Zach wakielekea shule iliyowekwa mapambo pamoja na chakula cha mchana huku marafiki wa Claire wanamsubiria kwa hamu matotokeo ya kura za Homecoming mpya. Claire amepuuza taratibu zote, lakini Zach ana mhamasisha atazame tangazo na aone kama kashinda au la. Kwa mshangao wa Claire, amechaguliwa kuwa Malkia wa Homecoming, na hasimu wake mkuu, Jackie Wilcox, ambaye mmoja wa wachaguzi wa kura. Amestaajabishwa, Claire na washabiki wengine wanazunguka na kutazama mili ya wanafunzi wengine wakitoa hongera zao za kumwunga mkono Claire.

Baadaye anagundua kwamba Zach ndiye aliyemfanyia kampeni za ushindi, kwa kufanya mpango wa ushindi kwa "kura kwa mtu asiyemaarufu" kwa kumfanya kila mtu ajue kwamba Claire si maarufu kama Jackie. Hata hivyo, Jackie, ameharibu wakati kwa majaribu ya kuchafua ushindi wa Claire kwa kumletea mzaha Zach. Claire, anaanza kujua umuhimu wa urafiki wa Zach kwake, ghafula anam-bamiza gumi la usoini Jackie.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]