Run!

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
"Run!"
Sehemu ya Heroes
Heroes s01e15.jpg
Matt Parkman almanusura afe baada ya Jessica kumtupa nje kupitia dirishani.
Sehemu ya. Msimu 1
Sehemu 15
Imetungwa na Adam Armus na Kay Foster
Imeongozwa na Roxann Dawson
Tayarisho la 115
Tarehe halisi ya kurushwa 12 Februari 2007
Waigizaji wageni
Wendo wa sehemu
← Iliyopita Ijayo →
"Distractions" "Unexpected"
Orodha ya sehemu za Heroes

"Run!" ni sehemu ya kumi na tatu ya msimu wa kwanza wa mfululizo wa igizo la ubunifu wa kisayansi linalorushwa hewani na kituo cha televisheni cha NBC, Heroes. Washiriki wa kawaida Milo Ventimiglia (Peter Petrelli) na Santiago Cabrera (Isaac Mendez) hawajaonekana kwenye kipengele hiki.

Hadithi[hariri | hariri chanzo]

Meredith anampigia simu Nathan na kumtaarifu kwamba binti yao Claire bado yu hai. Anatambua kwamba kashfa ya uzinzi inaweza kuharibu mpango mzima wa kisiasa hapo baadaye, Nathan anaamua kumpa Meredith $100,000 ili anyamaze kimya.

Penginepo, afya ya Mrs. Bennet inaanza kudhoofika, inasabisha mzozo baina ya Claire na Mr. Bennet, kwa kuwa anamlaumu Bennet kwa hali ya mama'ke. Anaamua kumpiga mkwara na kumwekea mipaka hakuna kutembea baada ya shule, hiyo imepelekea Claire kuwa na jazba mno.

Baadaye, Claire anaonekana kumwona Meredith kama msaliti, akiwa na matumaini ya kuwa baba'ke mzazi anaweza kumsaidia Bi. Bennet. Meredith anamwambia Claire kwamba atamsononesha tu, na Meredith mwenyewe anarudi zake mjini Mexico. Baada ya hapo, anampiga picha Claire ikiwa kama ukumbusho, ambayo baadaye alionesha kwa Nathan alipomtembelea.

Meredith kajitolea kuwatambulisha wote, lakini Nathan kakakataa - hii ilimshtua sana Claire aliyekuwa akisikiliza habari kwa kisiri. Alionekana ana huzuni, Nathan anaingia kwenye limo lake na kuondoka. Claire katupa jiwe kwenye kioo cha nyuma ya gari kwa hasira.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]