23 Septemba
Mandhari
(Elekezwa kutoka Septemba 23)
Ago - Septemba - Okt | ||||||
1 | 2 | 3 | 4 | 5 | 6 | 7 |
8 | 9 | 10 | 11 | 12 | 13 | 14 |
15 | 16 | 17 | 18 | 19 | 20 | 21 |
22 | 23 | 24 | 25 | 26 | 27 | 28 |
29 | 30 | |||||
Kalenda ya Gregori |
Tarehe 23 Septemba ni siku ya 266 ya mwaka (ya 267 katika miaka mirefu). Mpaka uishe zinabaki siku 99. Kwa kawaida ama ni sikusare otomnia ya kaskazini au siku ya kwanza baada ya sikusare hiyo. Katika nusutufe ya kaskazini ya dunia mchana huanza kuwa mfupi na muda wa usiku kuwa mrefu zaidi kuliko mchana. Kwenye nusutufe ya kusini mwendo ni kinyume: kuanzia sasa mchana hurefuka na giza la usiku kupungua. Mabadiliko hayo yanaonekana kote duniani kwenye umbali fulani kutoka ikweta.
Matukio
[hariri | hariri chanzo]- 1669 - Kuundwa kwa Chuo Kikuu cha Zagreb
Waliozaliwa
[hariri | hariri chanzo]- 1740 - Go-Sakuramachi, Mfalme Mkuu wa 117 wa Japani (1762-1771)
- 1771 - Kokaku, Mfalme Mkuu wa 119 wa Japani (1779-1817)
- 1901 - Jaroslav Seifert, mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fasihi mwaka wa 1984
- 1915 - Clifford Shull, mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fizikia mwaka wa 1994
- 1926 - John Coltrane, mwanamuziki kutoka Marekani
- 1949 - Bruce Springsteen, mwanamuziki kutoka Marekani
- 1960 - Mwenye heri Michał Tomaszek, O.F.M.Conv., padri mfiadini kutoka Poland aliyeuawa nchini Peru
- 1972 - Jermaine Dupri, mwanamuziki kutoka Marekani
Waliofariki
[hariri | hariri chanzo]- 1835 - Vincenzo Bellini, mtunzi wa opera kutoka Italia
- 1929 - Richard Zsigmondy, mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Kemia mwaka wa 1925
- 1968 - Mtakatifu Pio wa Pietrelcina, padri wa shirika la Ndugu Wadogo Wakapuchini kutoka Italia
- 1973 - Pablo Neruda, mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fasihi mwaka wa 1971
Sikukuu
[hariri | hariri chanzo]Wakristo wengi, wakifuata mapokeo ya Roma, huadhimisha kumbukumbu za watakatifu Pio wa Pietrelcina, Zakaria na Elisabeti, Papa Linus, Sosyo, Kostanso wa Ancona, Adomnani, Andrea, Yohane, Petro na Antoni, Kristofa, Antoni na Yohane n.k.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- BBC: On This Day
- On this day in Canada Archived 2012-12-09 at Archive.today
Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu 23 Septemba kama enzi zake au matokeo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |