Nenda kwa yaliyomo

Wakonventuali

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka O.F.M.Conv.)

Utawa wa Ndugu Wadogo Wakonventuali (kwa Kiingereza Order of Friars Minor Conventual, kifupi OFM Conv), au Wafransisko Wakonventuali, ni tawi la shirika la wanaume lililoanzishwa na Fransisko wa Asizi mwaka 1209.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Basilika la Mt. Fransisko, Assisi, ndilo kanisa kuu la Wafransisko wote. Linatunzwa na Wakonventuali likiwa na masalia ya mwanzilishi.

Wakati wa maisha ya mwanzilishi huyo, baadhi ya Ndugu Wadogo walianza kuishi mijini katika konventi kubwa.

Jambo hilo lilipingwa na wenzao waliopendelea mahali pa upwekeni na udogo katika majengo pia.

Ndiyo mwanzo wa farakano kati yao lililokamilika mwaka 1517, ambapo Papa aliwapa ushindi ndugu wa Observansya, yaani waliotaka kushika kikamilifu kanuni ya shirika.

Watakatifu wa shirika hilo ni Yosefu wa Kopertino, Fransisko Antonio Fasani na Maximilian Maria Kolbe.

Siku hizi idadi yao ni 4,500 hivi duniani kote.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]