Nenda kwa yaliyomo

Wakonventuali

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Utawa wa Ndugu Wadogo Wakonventuali (kwa Kiingereza Order of Friars Minor Conventual, kifupi: OFM Conv, au Wafransisko Wakonventuali) ni tawi la shirika la wanaume lililoanzishwa na Fransisko wa Asizi mwaka 1209.

Historia

[hariri | hariri chanzo]
Basilika la Mt. Fransisko, Assisi, ndilo kanisa kuu la Wafransisko wote. Linatunzwa na Wakonventuali likiwa na masalia ya mwanzilishi.

Wakati wa maisha ya mwanzilishi huyo, baadhi ya Ndugu Wadogo walianza kuishi mijini katika konventi kubwa.

Jambo hilo lilipingwa na wenzao waliopendelea makao ya upwekeni na udogo katika majengo pia.

Ndiyo mwanzo wa farakano kati yao lililokamilika mwaka 1517, ambapo Papa aliwapa ushindi ndugu wa Observansya, yaani waliotaka kushika kikamilifu kanuni ya shirika.

Watakatifu wa tawi hilo ni mapadri Yosefu wa Kopertino na Fransisko Antonio Fasani kutoka Italia Kusini na Maximilian Maria Kolbe kutoka Polandi.

Siku hizi idadi yao ni 4,500 hivi duniani kote.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu Kanisa Katoliki bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Wakonventuali kama historia yake au maelezo zaidi?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.