Nenda kwa yaliyomo

Uprotestanti

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Kiprotestanti)
Wahusika wakuu wa Matengenezo ya Kiprotestanti: Martin Luther na John Calvin wameonyesha katika mimbari ya kanisa la Mikolow, Poland.
Ramani inayoonyesha asilimia ya Waprotestanti kati ya wakazi wa kila nchi duniani.
Ramani inayoonyesha idadi ya Waprotestanti kwa kila nchi duniani mwaka 2010.      Zaidi ya milioni 150      Zaidi ya milioni 50      Zaidi ya milioni 20      Zaidi ya milioni 10      Zaidi ya milioni 5      More than 1 million


Uprotestanti ni aina ya Ukristo iliyotokana na Kanisa Katoliki huko Ulaya Kaskazini katika karne XVI kufuatana na tapo la kidini na la kisiasa maarufu kwa jina la "Matengenezo ya Kiprotestanti". Wahusika wakuu wa tapo hilo ni Martin Luther na Yohane Kalvini.

Asili

Martin Luther, daktari wa teolojia na padri mtawa, alisema kuwa Kanisa linapaswa kurejea kwenye mizizi yake, na kutoa uzito zaidi kwa yale yaliyoandikwa katika, Biblia. Luther alidhani kuwa Kanisa limekwenda mbali na mafundisho ya awali. Alichapisha tasnifu 95 kuhusu njia ya Kanisa Katoliki. Wengine wanasema, alizipigilia kwenye mlango wa kanisa la Wittenberg, lakini wengine wanasema hii si kweli. Tasnifu 95 zilichapishwa mnamo mwaka wa 1516 au 1517. Kwa maneno hayo, yalianza Matengenezo ya Kiprotestanti

== Jina ==. Mwaka 1529, Bunge la Speyer (Ujerumani), kikao cha wakuu wa Ujerumani na miji huru kilipokuwa kikiongea dhidi ya Matengenezo lilikataza tena uenezaji wake katika Dola Takatifu la Kiroma mpaka Mtaguso mkuu utakaporudisha utaratibu ndani ya Kanisa.

Lakini watawala waliomuunga mkono Luther walitoa hati ya pamoja inayoanza na maneno Protestamur, yaani Tunapinga.

Mwaka 1555 Amani ya Augsburg ilipitisha kauli ya kwamba cuius regio, eius religio, yaani kila raia anapaswa kufuata madhehebu ya eneo anamoishi, kadiri ilivyopangwa na mtawala wake, la sivyo ni lazima ahame.

Teolojia

Uprotestanti unagawanyika katika maelfu ya madhehebu tofauti, lakini inawezekana kutambua mambo kadhaa yanayolingana katika hayo yote:

Uenezi

Leo Waprotestanti wote duniani wanakadiriwa kuwa kati ya 800,000,000 na 1,000,000,000.

Tanbihi

Marejeo

  • Cook, Martin L. (1991). The Open Circle: Confessional Method in Theology. Minneapolis, Minn.: Fortress Press. xiv, 130 p. N.B.: Discusses the place of Confessions of Faith in Protestant theology, especially in Lutheranism. ISBN 0-8006-2482-3
  • Dillenberger, John, and Claude Welch (1988). Protestant Christianity, Interpreted through Its Development. Second ed. New York: Macmillan Publishing Co. ISBN 0-02-329601-1
  • McGrath, Alister E. (2007). Christianity's Dangerous Idea. New York: HarperOne.
  • Nash, Arnold S., ed. (1951). Protestant Thought in the Twentieth Century: Whence & Whither? New York: Macmillan Co.
  • Noll, Mark A. (2011). Protestantism: A Very Short Introduction. Oxford: Oxford University Press.

Viungo vya nje

Simple English Wiktionary
Simple English Wiktionary
Wikamusi ya Kiswahili ina dictionary definitions (word meanings):
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Uprotestanti kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.