Jimbo Katoliki la Mafinga
Mandhari
Jimbo Katoliki la Mafinga (kwa Kilatini "Dioecesis Mafingensis") ni mojawapo kati ya majimbo 35 ya Kanisa Katoliki nchini Tanzania na kama hayo yote linafuata mapokeo ya Kiroma.
Makao makuu yake yako Mafinga katika mkoa wa Iringa, lakini linaenea pia katika mkoa wa Mbeya (bonde la Usangu).
Kanisa kuu limewekwa wakfu kwa Kupalizwa Bikira Maria Mwenye Heri.
Kikanisa linahusiana na Jimbo Kuu la Mbeya.
Askofu wake wa kwanza ni Vincent Cosmas Mwagala.
Historia
[hariri | hariri chanzo]- 23 Desemba 2023: Kuanzishwa kutokana na Jimbo Katoliki la Iringa
Takwimu
[hariri | hariri chanzo]Wakati wa kuanzishwa, eneo lake lilikuwa la kilometa mraba 11,016, ambapo kati ya wakazi 617,770, Wakatoliki ni 236,299 (38.3%) katika parokia 17. Mapadri ni 41, wakiwemo wanajimbo 30 na watawa 11. Kwa wastani kila mmoja anahudumia waamini 5,763. Mabruda ni 5 na masista 136.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]Makala hii kuhusu Kanisa Katoliki bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Jimbo Katoliki la Mafinga kama historia yake au maelezo zaidi? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |