Ijumaa Kuu
Mwaka wa liturujia |
---|
Magharibi |
Mashariki |
Ijumaa Kuu ni siku ya Ijumaa kabla ya Pasaka ambapo Wakristo wengi duniani wanaadhimisha kifo cha Yesu Kristo msalabani.
Kufuatana na taarifa za Injili nne katika Biblia ya Kikristo, Yesu alisulubiwa siku kabla ya Sabato (au Jumamosi), yaani Ijumaa. Mahali pa kumsulubisha palikuwa kilima cha Golgotha kilichokuwepo wakati ule nje ya kuta za mji wa Yerusalemu.
Tarehe
[hariri | hariri chanzo]Kadiri ya Injili ya Mtume Yohane, kesho yake ilikuwa Sabato na pia Pasaka, jambo lisilotokea kila mwaka. Kwa sababu hiyo wataalamu mbalimbali wameweza kukadiria ilikuwa tarehe 7 Aprili 30.
Sikukuu hii haina tarehe thabiti katika kalenda ya kawaida. Ilhali hutangulia Pasaka inafuata pia mabadiliko ya tarehe za Pasaka. Pamoja na mapokeo yaliyo tofauti kati ya Ukristo wa Magharibi (Wakatoliki na Waprotestanti wengi) na Ukristo wa Mashariki (makanisa ya Kiorthodoksi na Wakatoliki wa Mashariki), kuna tarehe mbili tofauti za Pasaka, na hivyo pia kila mwaka kuna tarehe mbili tofauti za Ijumaa Kuu.
Mwaka | Ukristo wa Magharibi |
Ukristo wa Mashariki |
---|---|---|
2018 | 30 Machi | 06 Aprili |
2019 | 19 Aprili | 26 Aprili |
2020 | 10 Aprili | 17 Aprili |
2021 | 02 Aprili | 30 Aprili |
2022 | 15 Aprili | 22 Aprili |
Katika liturujia ya makanisa
[hariri | hariri chanzo]Ijumaa kuu ni sehemu ya Juma Kuu linaloanza kwa adhimisho la Yesu kuingia mji huo akishangiliwa kama mfalme wa Wayahudi (yaani Masiya au Kristo). Adhimisho hilo linafanyika mwanzoni mwa wiki, yaani Jumapili ya matawi.
Ijumaa kuu ni pia sehemu ya siku tatu kuu za Pasaka zinazoadhimisha mateso na kifo chake (Ijumaa), kulala kaburini (Jumamosi), na hatimaye kufufuka kwa utukufu (Jumapili), kwa ufupi:
- Yesu mteswa,
- mzikwa na
- mfufuka.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Commentary on Luke's account of the trial and death of Jesus from InterVarsity Press
- Good Friday on RE:Quest Ilihifadhiwa 17 Aprili 2009 kwenye Wayback Machine.
- The Eastern Orthodox commemoration of Holy Friday Ilihifadhiwa 7 Juni 2011 kwenye Wayback Machine.
- Great Friday Ilihifadhiwa 24 Aprili 2011 kwenye Wayback Machine. instructions from S. V. Bulgakov's Handbook for Church Servers (Waorthodoksi Warusi)
- "Good Friday" article from The Catholic Encyclopedia
- Good Friday Celebrations Ilihifadhiwa 7 Januari 2010 kwenye Wayback Machine.
- Episcopal Good Friday Service
- Presbyterian Good Friday Service Ilihifadhiwa 25 Machi 2009 kwenye Wayback Machine.
- Good Friday hymns at St-Takla.org (Wakopti)
- The Text This Week: Good Friday
Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Ijumaa Kuu kama historia yake, matokeo au athari zake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |