Uislamu mjini Zanzibar

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Uislamu kwa nchi

Uislamu ndiyo dini kubwa katika kisiwa cha Zanzibar. Kwa mujibu wa CIA Factbook, Zanzibar ina Waislamu zaidi ya 99%. Uislamu uliingia mjini Zanzibar kunako karne ya 10.

Uislamu katika harakati za kupinga ukoloni[hariri | hariri chanzo]

Kwa mujibu wa chanzo kimoja, "Uislamu mjini Zanzibar imetia msukumo harakati za kupinga ukoloni, kisiasa na hata kitaifa wakati wa kupigania uhuru." [1]

Harakati za Uamsho[hariri | hariri chanzo]

Ni jumuiya ya wanaharakati wa Kiislamu wa Zanzibar (Association for Islamic Mobilisation and Propagation)[2] ambayo ina mpango wa kupigania uhuru wa Zanzibar kutoka mikononi mwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania [3] pia wanajulikana kama JUMIKI au Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislam. JUMIKI walisajiliwa rasmi mnamo mwaka wa 2001 huko mjini Zanzibar na Nambari yao ya Usajili ni 149 chini ya kifungu cha 6 cha mwaka wa 1995 kuhusiana na Taasisi za Kijamii.

Mipango[hariri | hariri chanzo]

1) Zanzibar irudi katika asili yake ya zamani kuwa kitovu cha dini ya Uislamu na taasisi. 2) Kuhakikisha sheri za Kiislamu zinatekelezwa. 3) Kuhakikisha Kuipa Uhuru Zanzibar wa kujiamulia mambo yake yenyewe.

Taasisi imeanza kampeni zake katika maeneo tofauti ya mikoa huko mjini Zanzibar ikiwa na lengo la kudai uhuru wa Zanzibar kutoka mikononi mwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Uamsho waliitisha kura ya maoni juu ya kujitoa kwa Zanzibar katika muungano wake na Tanzania bara, kitendo ambacho kimepelekea kwa serikali zote mbili ya Tanzania bara na Visiwani kuingilia kati na kuzuia mikutano yote ya aina hiyo, kwa kuwaambia hakuna kufanya mikutano yoyote hadi hapo taarifa zaidi zitakapotolewa.[4].

Uharibifu kadhaa uliripotiwa na jumuia hiyo ikiwa ni pamoja na suala la kuchoma makanisa mawili huko mjini Zanzibar, Polisi wakawashtaki kundi Uamsho kwa kutoa agizo la kufanya hivyo kupitia wafuasi wake huko mitaani - lakini viongozi wa jumuia hiyo walikataa kuhusishwa na matukio hayo.[5][6]

Baadhi ya watafiti walieleza kwamba kikundi cha kina Uamsho kimepata umaarufu wake baada ya kutiwa jeuri na msaada wa chama kikubwa cha upinzani cha mjini Zanzibar cha Civic United Front (CUF) hasa baada ya uamuzi wake kutaka kuanzishwa kwa serikali ya muungano na chama tawala cha Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-02-06. Iliwekwa mnamo 2012-08-23. 
  2. https://uamshozanzibar.wordpress.com/kuhusu-uamsho/
  3. https://uamshozanzibar.wordpress.com/kuhusu-uamsho/
  4. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-05-31. Iliwekwa mnamo 2012-08-23. 
  5. http://wolfganghthome.wordpress.com/2012/05/28/zanzibar-clashes-see-two-churches-burnt-and-running-battles-between-islamic-radicals-and-security-forces/
  6. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-05-31. Iliwekwa mnamo 2012-08-23.  Unknown parameter |= ignored (help)

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]