Chuo Kikuu Huria cha Tanzania
Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (kwa Kiingereza: Open University of Tanzania) ni chuo kikuu kinachotoa kozi za cheti, stashahada na shahada kupita masomo ya mbali (Distance Learning). Makao makuu yako Dar es Salaam, Tanzania. Chuo Kikuu Huria kina takribani wanafunzi 70,000 kutoka ngazi mbalimbali za kitaaluma.
Historia
[hariri | hariri chanzo]Kilianzishwa mwaka 1992 kwa kilichoanzishwa kwa Sheria ya Bunge namba 17 ya mwaka 1992. Sheria hiyo ilipata nguvu ya utendaji rasmi tarehe 1 Machi 1993 kwa mujibu wa tangazo la serikali namba 55 ya gazeti lake rasmi.
Mwaka 1994, Januari 19 Makamu Mkuu wa kwanza wa Chuo alishika madaraka na mwezi huohuo walisajiliwa wanafunzi wa awamu ya kwanza.
Mwaka 2007 kwa mujibu wa sheria ya vyuo vikuu, Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kilianza kutumia sheria na taratibu zake za ndani ya chuo toleo la mwaka (2007) katika shughuli zake za kiutawala [1].
Taaluma
[hariri | hariri chanzo]Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kinatoa stashahada, diploma na shahada mbalimbali kupitia elimu ya kimtandao au elimu ya masafa ya juu kwa njia ya tehama au nyenzo nyingine mbalimbali za kiteknolojia. Shughuli za chuo zinafanyika na kutoa huduma katika viwango vya utendaji na usimamiaji wa baraza la vyuo vikuu Tanzania (TCU). Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kinatoa programu takribani 125.
Vituo
[hariri | hariri chanzo]Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kina vituo kwenye mikoa zaidi ya 30 nchini Tanzania; hii ni kujumlisha na vituo vya Jamhuri ya Watu wa Zanzibar (Unguja na Pemba), Kenya vituo viwili (Chuo cha Egerton na Njoro), Rwanda (eneo la Kibungo), Uganda na Namibia (Chuo cha Triumph).
Vituo vingine vya mashirikiano ya ndani ni ACDE-TCC (African Council for Distance Education- Technical Collaboration Committee), CECED (Centre for Economics and Community Economic Development), SADC ODL CoS TE (SADC Centre of Specialization in Teacher Education).
Chuo Kikuu Huria kina vituo vya kusomea takribani 69 ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Vitivo
[hariri | hariri chanzo]Ina:
- Kitivo cha Sanaa na Sayansi ya Jamii
- Kitivo cha Elimu
- Kitivo cha Sheria
- Kitivo cha Uongozi wa Biashara
- Kitivo cha Sayansi, Teknolojia na Masomo ya Mazingira
- Taasisi ya kuyaendeleza masomo
- Taasisi ya Teknolojia ya Elimu
- Kurugenzi ya Huduma za Mikoa
- Kurugenzi ya Utafiti na Masomo ya baada ya Shahada
Watu maarufu waliohitimu chuoni
[hariri | hariri chanzo]- Jakaya Kikwete, Rais wa awamu ya nne wa Tanzania
- Benjamin Mkapa, Rais wa awamu ya tatu wa Tanzania
- Ali Hassan Mwinyi, Rais wa awamu ya pili wa Tanzania
- Samia Suluhu, Rais wa awamu ya sita wa Tanzania
- William Lukuvi, Mbunge na Waziri wa Serikali ya Tanzania
- Constantine Kanyasu, Mbunge na Naibu Waziri wa Serikali ya Tanzania
- Asha Abdullah Juma, Mbunge na Waziri mstaafu Serikali ya Tanzania
- Angeline Mabula, Mbunge na Waziri wa Serikali ya Tanzania
- Mary Machuche Mwanjelwa, Mbunge na Naibu Waziri Serikali ya Tanzania
- Irene Tarimo, Mtafiti na Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu Huria cha Tanzania
- Stella Martin Manyanya, Mbunge na Naibu Waziri wa Serikali ya Tanzania
- George Boniface Simbachawene, Mbunge na Waziri wa Serikali ya Tanzania
- Vedastus Mathayo Manyinyi, Mbunge wa Kitaifa nchini Tanzania
- Khadija Nassir Ali, Mbunge wa Kitaifa nchini Tanzania
- Fatma Hassan Toufiq, Mbunge wa Kitaifa nchini Tanzania
- Taska Restituta Mbogo, Mbunge wa Kitaifa nchini Tanzania
- Wanu Hafidh Ameir, Mbunge wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar
- Mary Deo Muro, Mbunge wa Kitaifa nchini Tanzania
- Emmanuel Adamson Mwakasaka, Mbunge wa Kitaifa nchini Tanzania
- Sebastian Simon Kapufi, Mbunge wa Kitaifa nchini Tanzania
- Cecilia Daniel Paresso, Mbunge wa Kitaifa nchini Tanzania
- Joseph Michael Mkundi, Mbunge wa Kitaifa nchini Tanzania
- Jeremia Maselle Bukwimba, Mbunge wa Kitaifa nchini Tanzania
- Lucia Ursula Michael Mlowe, Mbunge wa Kitaifa nchini Tanzania
- Augustino Manyanda Masele, Mbunge wa Kitaifa nchini Tanzania
- Grace Victor Tendega, Mbunge wa Kitaifa nchini Tanzania
- Khamis Mtumwa Ali, Mbunge wa Kitaifa nchini Tanzania
- Munde Abdallah Tambwe, Mbunge wa Kitaifa nchini Tanzania
- Jacqueline Kandidus Ngonyani, Mbunge wa Kitaifa nchini Tanzania
- Jamal Kassim Ali, Mbunge wa Kitaifa nchini Tanzania
- Philipo Augustino Mulugo, Naibu Waziri wa Serikali ya Tanzania
- Maryam Salum Msabaha, Mbunge wa Kitaifa nchini Tanzania
- Makame Kassim Makame, Mbunge wa Kitaifa nchini Tanzania
- Almas Athuman Maige, Mbunge wa Kitaifa nchini Tanzania
- Joram Ismael Hongoli, Mbunge wa Kitaifa nchini Tanzania
- Shamsi Vuai Nahodha, Waziri Kiongozi Serikali ya Mapinduzi Zanzibar
- Peya Mushelenga, Mshairi na Mwanasiasa wa nchini Namibia
- Haji Faki Shaali, Waziri katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar
- Mohamed Ramia Abdiwawa, Balozi na Waziri katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar
- Amir Nondo, Meya Mstaafu wa Manispaa ya Morogoro Mji.
- Maftaha Abdallah Nachuma, Mbunge wa Kitaifa nchini Tanzania
- Maryam Salum Msabaha, Mbunge wa Kitaifa nchini Tanzania
- Mashimba Mashauri Ndaki, Waziri wa Kitaifa nchini Tanzania
- Hashil Abdallah, Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Miss Excellence Tanzania
- Wavuti rasmi ya Shule Archived 18 Novemba 2019 at the Wayback Machine.
- Chuo Kikuu cha Afrika Kusini Archived 28 Julai 2011 at the Wayback Machine.
Makala hii kuhusu mambo ya elimu bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kama historia yake, uenezi au maendeleo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |