Irene Tarimo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search


Daktari
Irene Tarimo
Mhadhiri
Amezaliwa01 Oktoba 1964
UtaifaMtanzania
Majina mengineIrene Aurelia Tarimo
ElimuSekondari ya Kilakala, Sekondari ya Weruweru, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Chuo Kikuu Huria cha Tanzania
Kazi yakeMhadhiri na Mkuu wa Idara Chuo Kikuu Huria cha Tanzania
NduguJaji John Mrosso

Irene Aurelia Tarimo (amezaliwa 1964) ni Mhadhiri nchini Tanzania, na Mkuu wa Idara ya Masomo ya Sayansi ya Mazingira katika Chuo Kikuu Huria cha Tanzania [1]. Pia ni mwanasayansi na mtafiti katika Chuo Kikuu Huria cha Tanzania [2]. Alikuwa Mkurugenzi wa Kituo cha mkoa wa Lindi wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kwa karibu miaka tisa.

Wasifu[hariri | hariri chanzo]

Irene alimaliza elimu yake ya awali ya msingi Rombo. Katika elimu yake ya sekondari alikuwa mwanafunzi katika shule ya wasichana ya Weruweru iliyopo mjini Kilimanjaro na baadae kujiunga kidato cha tano na sita na shule ya wasichana ya Kilakala iliyopo Morogoro. Alijiunga na chuo cha ualimu cha Dar es Salaam DUCE na kusoma masomo ya kemia, biolojia na taaluma. Alipomaliza alipata ajira ya ualimu katika shule za sekorandari, Shule ya Sekondari ya Kifungilo, Shule ya Sekondari ya Morogoro, Shule ya Sekondari ya Weruweru na Shule ya Sekondari ya Mwika.

Mwaka 1995 alijiunga Chuo Kikuu Huria cha Tanzania na mwaka 2003 alitunukiwa shahada ya kwanza ya sayansi katika taaluma (B.Sc.Ed) kwa daraja la kwanza. Irene aliweka historia kwa kuwa mwanafunzi wa kwanza tangu miaka kumi ya kuanzishwa Chuo Kikuu Huria mwaka 1992 kupata alama ya daraja la kwanza. Alipata zawadi kutuka kwa makamu mkuu wa chuo na waziri wa elimu, sayansi na teknolojia.

Irene alijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa masomo ya shahada ya pili ya uzamili katika sayansi ya mazingira na kuhitimu mwaka 2007. Baadaye alijiunga tena na Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kwa shahada ya tatu ya uzamivu mpaka kumaliza kwake mwaka 2013.

Mahafali ya kuhitimu Dk. Irene Tarimo OUT, akiwa na Prof. Tolly Mbwette

Kazi[hariri | hariri chanzo]

Daktari Irene amekuwa Mkurugenzi wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, mkoa wa Lindi kwa takribani miaka tisa tangu 2007 amewezesha shughuli za chuo ukanda wa mikoa ya kusini mwa Tanzania kufanikiwa kwa ustadi na uadilifu mkubwa. Amewezesha kituo cha Lindi kupata eneo la ardhi takribani ekari 100 kwa ajili ya upanuzi wa ujenzi wa makazi mapya ya kituo cha chuo. Pia alifanikisha upatikanaji wa ekari takribani 3 kwa ajili ya maonyesho ya nane nane eneo la Ngongo, mkoani Lindi [3]. Alifanikisha harambee ya upatikanaji gari la usafiri wa chuo na kwa shughuli nyingine mbalimbali za chuo [4].

Dkt. Irene Tarimo na Salma Kikwete kwenye mahafali

 

Machapisho[hariri | hariri chanzo]

Irene Aurelia Tarimo ameandika machapisho kadhaa juu ya sayansi na mambo ya kijamii: