Salma Kikwete

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search


Salma Kikwete
Amezaliwa30 Novemba 1963 (1963-11-30) (umri 56)
UtaifaTanzania
CheoMke wa Rais wa Tanzania
Chama cha siasaCCM
NdoaJakaya Kikwete (m. 1989–present) «start: (1989)»"Marriage: Jakaya Kikwete to Salma Kikwete" Location: (linkback://sw.wikipedia.org/wiki/Salma_Kikwete)
Watoto5

Salma Kikwete (alizaliwa tarehe 30 Novemba 1963) ni mwalimu, mwanaharakati na mwanasiasa ambaye ni mke wa aliyekuwa Rais wa Tanzania wa awamu ya nne Jakaya Mrisho Khalfan Kikwete[1], madarakani kuanzia mwaka 2005 hadi 2015.

Awali Salma Kikwete alifanya kazi kama mwalimu kwa zaidi ya miaka ishirini.[1]

Mwaka wa 2005, serikali ilianzisha kampeni ya taifa ya upimaji wa hiari wa virusi vya UKIMWI jijini Dar es Salaam. Salma Kikwete na mumwe walikuwa wa kwanza kupimwa nchini humo.[2]

Mwaka wa 2009, alikuwa Makamu wa Rais wa Kanda ya Mashariki wa Jumuiya ya Wake wa Marais wa Afrika dhidi ya UKIMWI (Organization of African First Ladies Against AIDS - OAFLA).[1]

Mwaka 2012, Salma Kikwete, Rais wa zamani wa Botswana Festus Mogae na watu wengine kumi mashuhuri barani Afrika waliungana na UNESCO na UNAIDS kuunga mkono mkakati wa Mashariki na Kusini mwa Afrika wa Kuzuia Maambukizi ya Virusi vya UKIMWI na Afya ya Kijinsia kwa Watoto Wadogo, ambayo ilianzishwa tangu Novemba 2011.[3]

Kikwete pia ni mwanzilishi wa Wanawake na Maendeleo (WAMA), shirika lisilo la kiserikali ambalo linachochea maendeleo ya wanawake na watoto.[1]

Mwaka mmoja baada ya mumewe kuondoka madarakani, Salma Kikwete alichaguliwa na Rais John Magufuli kuwa mbunge wa viti maalumu tarehe 1 Machi 2017.[4]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. 1.0 1.1 1.2 1.3 "Her Excellency Salma Kikwete", Jamaica Information Service, 2009-11-23. Retrieved on 2012-08-09. 
  2. "Tanzanian leader takes Aids test", BBC News, 2007-07-14. Retrieved on 2012-07-30. 
  3. "Leaders to lobby for HIV Prevention and Sexual Health for Youth in Eastern and Southern Africa", UNESCO, 2012-06-27. Retrieved on 2012-07-30. 
  4. Esther Karin Mngodo, "The Salma Kikwete story", The Citizen, 3 March 2017.