Maria Nyerere

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Maria Nyerere

Maria (kulia) na Evelyn Macleod

Mke wa rais wa kwanza wa Tanzania
Muda wa Utawala
29 Oktoba 1964 – 5 Novemba 1985
mtangulizi Mwanzilishi
aliyemfuata Siti Mwinyi

Mke wa rais wa Tanganyika
Muda wa Utawala
9 Disemba 1962 – 25 Aprili 1964

tarehe ya kuzaliwa 31 Desemba 1930 (1930-12-31) (umri 93)
Tanganyika
utaifa Mtanzania
chama Chama Cha Mapinduzi
ndoa Julius Nyerere (1953-1999)
watoto
mhitimu wa Sumve Teacher Training College
Fani yake Mwalimu
dini Mkristo - Katoliki

Maria Nyerere (alizaliwa kama Maria Waningu Gabriel Magige[1] mnamo 31 Disemba 1930[2][3]) alikuwa mke wa rais wa kwanza wa Tanzania Mwl Julius Kambarage Nyerere kuanzia 1964 hadi 1985.[4] Kwa kawaida nchini Tanzania anajulikana kama 'Mama Maria' tu.[5][6]

Alikuwa mtoto wa saba kati ya tisa wa Gabriel Magige, wa Baraki, Tareme[7], kutoka kwa mkewe Hannah Nyashiboha.[8]

Maria alisoma katika shule "White Sisters' School" iliyokuwa Nyegina, kisha shule ya Ukerewe, kisha akajiunga na chuo cha ualimu "Sumve Teacher Training College"; alihitimu kwa kupata cheti cha ualimu akaanza kufundisha katika Shule ya Msingi Nyegina iliyoko Musoma.[9] Aliolewa na Julius Nyerere mwaka 1953.

Kwa sasa ni miongoni mwa wajumbe saba wa baraza la wazee wa "Alliance for Tanzania Youth Economic Empowerment" (Atyee), pamoja na rais wa zamani wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ali Hassan Mwinyi na rais wa zamani wa Zanzibar Amani Abeid Karume ambaye alikuwa mtoto wa Rais wa kwanza wa Zanzibar.[10]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Nyerere and Africa: End of an Era, Godfrey Mwakikagile, New Africa Press, 2007, pg 403
  2. https://mobile.twitter.com/tanzaniahistory/status/815211458787209216
  3. Nyerere: The Early Years, Thomas Molony, 2014, pg 89
  4. Profile: Nyerere. juliusnyerere.info. Jalada kutoka ya awali juu ya 1 July 2013. Iliwekwa mnamo 23 May 2013.
  5. http://www.monitor.co.ug/Magazines/Full-Woman/Mama-Maria--Keeping-Mwalimu-Julius-Nyerere-s-candle-alight/-/689842/2346950/-/38nwks/-/index.html
  6. Nakala iliyohifadhiwa. Jalada kutoka ya awali juu ya 2015-07-22. Iliwekwa mnamo 2018-05-19.
  7. Nyerere and Africa: End of an Era, Godfrey Mwakikagile, New Africa Press, 2007, pg 628
  8. Nyerere: The Early Years, Thomas Molony, 2014, pg 89
  9. Nyerere: The Early Years, Thomas Molony, 2014, pg 90
  10. Nakala iliyohifadhiwa. Jalada kutoka ya awali juu ya 2015-07-21. Iliwekwa mnamo 2018-05-19.