Nenda kwa yaliyomo

Shahada ya Awali

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Shahada ya awali)
Vazi maalumu linalovaliwa na wahitimu wa ngazi ya Bachelor Degree

Shahada ya awali (pia: Digrii ya bachelor [1]) ni shahada ya kwanza inayotolewa kwa mwanafunzi wa chuo kikuu aliyefaulu masomo ya fani fulani katika muda wa miaka mitatu au minne, kutegemeana na nchi na mfumo wa chuo.

Katika nchi zinazofuata mfumo wa Uingereza ni miaka mitatu, kwenye mfumo wa Marekani ni muda wa miaka minne kutokana na tofauti katika kiwango cha elimu ya sekondari.

Nchi nyingine hazina digrii hiyo kwa sababu kwao masomo ya chuo kikuu hupangwa kwa muda wa miaka mitano hadi sita tangu mwanzo.

Vyeo vinavyofuata ni digrii ya uzamili (au "umahiri", "masters") na digrii ya uzamivu ("udaktari").

  1. Neno "bachelor" kwa lugha ya Kiingereza kimsingi linataja mtu asiyeoa bado lakini mwenye umri wa kutosha.