Fatma Hassan Toufiq

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Fatma Hassan Toufiq (amezaliwa 29 Februari 1960) ni mwanasiasa Mtanzania na mwanachama wa Chama cha kisiasa cha [[Chama Cha Mapinduzi] (CCM). Amechaguliwa kuwa mbunge wa Viti maalum vya wanawake kwa miaka 20152020. [1]

Alipata elimu yake ya msingi katika shule ya msingi Mtekelezo (1967-1973) na elimu ya sekondari katika shule ya sekondari Central (1974-1977). Alipata cheti cha ualimu katika Chuo cha ualimu Marangu (1979-1981) na (2009-2013) alisomea shahada ya kwanza katika Chuo Kikuu Huria cha Tanzania na shahada ya uzamili (2014-2016) katika Chuo Kikuu Huria cha Tanzania. [2]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Tovuti ya Bunge la Tanzania, iliangaliwa Mei 2017
  2. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-01-26. Iliwekwa mnamo 2020-01-26.