Mkoa wa Mbeya
Mkoa wa Mbeya |
|
Mahali pa Mkoa wa Mbeya katika Tanzania | |
Majiranukta: 2°45′S 32°45′E / 2.750°S 32.750°E | |
Nchi | Tanzania |
---|---|
Wilaya | 8 |
Mji mkuu | Mbeya |
Serikali | |
- Mkuu wa Mkoa | John L. Mwakipesile |
Eneo | |
- Jumla | 63,617 km² |
Idadi ya wakazi (2002) | |
- Wakazi kwa ujumla | 2,070,046 |
Tovuti: http://www.mbeya.go.tz/ |
Mkoa wa Mbeya ni kati ya mikoa 26 ya Tanzania ikipakana na Zambia na Malawi, halafu na mikoa ya Rukwa, Tabora, Singida na Iringa.
Kuna wilaya 8 zifuatazo: Mbeya Mjini, Mbeya Vijijini, Rungwe, Kyela, Ileje, Mbozi, Chunya na Mbarali.
Mbeya ni kati ya maeneo yanayopendeza kabisa ndani ya Tanzania ikiwa na sehemu za Ziwa la Nyasa, Ziwa Rukwa, milima ya Mbeya, milima ya Rungwe, Uwanja wa juu wa Uporoto, Uwanja wa Usangu ingawa haukufikiwa bado na utalii.
Wenyeji wa wilaya ya Chunya ni Wabungu na waishio huko zaidi ni Wanyiha.
Wilaya ya Rungwe ni eneo penye mvua nyingi katika Tanzania. Mkoa wa ujumla ni mojawapo kati ya mikoa yenye kilimo kizuri inayotoa mazao ya kulisha taifa. Lakini maeneo makubwa ya Wilaya ya Chunya ni makavu.
Wilaya ya Chunya ina madini mbalimbali hasa dhahabu. Mbeya na Mbozi kahawa hupandwa. Rungwe pana chai nyingi, pamoja na Rungwe na Chimala hulimwa mpunga. Nyanda za juu kuna nafaka na viazi.
Kijiolojia mkoa wa Mbeya ni eneo la kukutana kwa mikono miwili ya Bonde la Ufa la Afrika ya Mashariki inayoendelaea hapa katika ziwa Nyasa.
Maziwa na mito
Mkoa wa Mbeya inapakana na maziwa mawili makubwa ndiyo Ziwa Nyasa na Ziwa Rukwa. Hasa milima yenye asili ya volkeno ya wilaya ya Rungwe inyajaa maziwa ya kasoko.
Mito mikubwa ni Songwe na Kiwira. Chanzo ya mto Ruvuma iko pia Mbeya katika tambarare ya Usangu.
Viungo vya nje
- Mbeya Region Socioeconomic Profile katika TZOnline (Kiingereza)
Arusha | Dar es Salaam | Dodoma | Geita | Iringa | Kagera | Katavi | Kigoma | Kilimanjaro | Lindi | Manyara | Mara | Mbeya | Morogoro | Mtwara | Mwanza | Njombe | Pemba Kaskazini | Pemba Kusini | Pwani | Rukwa | Ruvuma | Shinyanga | Simiyu | Singida | Songwe | Tabora | Tanga | Unguja Kaskazini | Unguja Kusini | Unguja Mjini Magharibi |