Jina takatifu la Maria

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Bibi Yetu wa Mawaridi alivyochorwa na William-Adolphe Bouguereau (1825-1905).

Jina takatifu la Maria ni kumbukumbu ya hiari katika kalenda ya liturujia ya Kanisa la Kilatini. Huadhimishwa tarehe 12 Septemba.

Historia ya adhimisho[hariri | hariri chanzo]

Iliingizwa na Papa Innocent XI mwaka 1684, kufuatana na ushindi wa Wakristo dhidi ya Waturuki Waislamu katika Mapigano ya Vienna (1683).[1]

Baada ya Mtaguso wa pili wa Vatikano ilitolewa, lakini ilirudishwa tena na Papa Yohane Paulo II mwaka 2002, pamoja na kumbukumbu ya Jina takatifu la Yesu.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Ann Ball, 2003 Encyclopedia of Catholic Devotions and Practices ISBN 0-87973-910-X page 242

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Christianity Symbol.png Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Jina takatifu la Maria kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.