Jimbo Kuu la Dodoma
Mandhari
Jimbo Kuu la Dodoma (kwa Kilatini Archidioecesis Dodomaensis) ni mojawapo kati ya majimbo 36 ya Kanisa Katoliki nchini Tanzania na kama hayo yote linafuata mapokeo ya Kiroma.
Kikanisa lina majimbo ya Kondoa na Singida chini yake.
Askofu mkuu wake ni Beatus Kinyaiya, O.F.M.Cap.
Historia
[hariri | hariri chanzo]- 1935: Kuanzishwa kwa Apostolic Prefecture ya Dodoma kutokana na Apostolic Vicariate ya Bagamoyo
- 1951: Kupandishwa cheo kuwa Apostolic Vicariate ya Dodoma
- 1953: Kufanywa dayosisi
- 6 Novemba 2014: Kupandishwa cheo na kuwa jimbo kuu.
Uongozi
[hariri | hariri chanzo]- Maaskofu wakuu wa Dodoma
- Beatus Kinyaiya, O.F.M.Cap.
- Maaskofu wa Dodoma
- Gervas John Mwasikwabhila Nyaisonga (2011-2013)
- Jude Thadaeus Ruwa’ichi OFMCap (2005 – 2010)
- Matthias Joseph Isuja (1972 – 2005)
- Anthony Jeremiah Pesce CP (1953 – 1971)
- Vicar Apostolic wa Dodoma
- Anthony Jeremiah Pesce CP (1951 – 1953)
- Prefect Apostolic wa Dodoma
- Padri Stanislao dell’Addolorata CP (1937 – 1941)
Takwimu
[hariri | hariri chanzo]Eneo ni la kilometa mraba 41,311, ambapo kati ya wakazi 1,908,000 (2006) Wakatoliki ni 398,000 (20.9%).
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]![]() |
Makala hii kuhusu Kanisa Katoliki bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Jimbo Kuu la Dodoma kama historia yake au maelezo zaidi? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |