Nenda kwa yaliyomo

Historia ya maeneo ya Pasifiki

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kanda ndani ya maeneo ya Australia na visiwa vya Pasifiki.

Historia ya maeneo ya Pasifiki inahusu historia ya watu kwenye visiwa vya Pasifiki. Historia hiyo huangaliwa kufuatana na kanda zake kama vile Polinesia, Melanesia na Mikronesia; mara nyingi inaangaliwa pamoja na Australia na Nyuzilandi (ing. History of Oceania).

Ugunduzi na wakazi wa kwanza

[hariri | hariri chanzo]
Mtoto wa Vanuatu

Historia ya maeneo ya Pasifiki ilianza na uhamiaji wa wanadamu walioenea huko angalau miaka 40,000 iliyopita. Walitokea Asia ya Kusini-Mashariki wakafika Australia na Guinea Mpya pamoja na visiwa kadhaa vya Melanesia, lakini eneo kubwa la visiwa vilivyotawanyika katika Bahari Pasifiki lilikuwa halijakaliwa na watu bado.

Watu walianza kuenea huko mnamo 1500 KK - 1300 KK: uwezekano mkubwa ni kwamba walitokea mwanzoni Ufilipino na Taiwan. Katika mwendo wa karne nyingi wahamiaji walifikia kisiwa kimoja baada ya kingine na kupanua eneo la makazi zaidi upande wa mashariki.

Wapolinesia walifika kwenye pembetatu ya Tonga - Fiji - Samoa wakaendelea kwa safari za mbali wakiwa na mitumbwi yao hadi kufikia Hawaii, Nyuzilandi na mashariki mwa Pasifiki mpaka Kisiwa cha Pasaka.

Historia ya uenezi huo ni vigumu kuifanyia utafiti kwa sababu watu hao hawakuwa na maandishi. Ni mila chache tu za mdomo ambazo zimeendelea kuhifadhiwa hadi nyakati za kisasa, kama vile kuhusu makazi ya kwanza New Zealand yaliyoanzishwa na Tama Te Kapua.

Taarifa zilizoandikwa zinapatikana tu tangu kufika kwa Wazungu wa kwanza katika karne ya 16.

Karne ya 16

[hariri | hariri chanzo]
Safari ya Magellan alipozunguka Dunia yote kwenye karne ya 16.

Katika karne hiyo Wareno na Wahispania walikuwa Wazungu wa kwanza kusafiri katika Bahari Pasifiki. Waliwahi kufika Amerika kuanzia Kristoforo Kolumbus wakitafuta njia ya kufika China na Uhindi wakihamasishwa na shabaha za kibiashara na za kisiasa; walitaka kuanzisha biashara ya moja kwa moja na matajiri wa Mashariki bila kulazimishwa kulipa bei za juu za wafanyabiashara Waislamu waliotawala biashara hiyo hadi wakati ule.

Mwisho wa karne ya 16 na katika karne ya 17 hao wa kwanza walifuatwa na Waholanzi, Waingereza na Wafaransa.

Wapelelezi Wazungu

[hariri | hariri chanzo]
Ngoma ya vita ya Wamaori; wenyeji hao wa Nyuzilandi walipigana na Waingereza walipovamia visiwa vyao.

Karne ya 19 na ukoloni

[hariri | hariri chanzo]

Nchi za Ulaya na Amerika ziliendelea kutuma meli za upelelezi zinazochora ramani na kukusanya data kuhusu visiwa na watu wao. Katika karne ya 19 ubeberu unaanza kuathiri hali. Visiwa ambavyo hadi sasa havikuwa na umuhimu wa kibiashara wala wa kijeshi vinaangaliwa upya. Wajasiriamali Wazungu wanafika kwenye visiwa kadhaa wakianza kununua ardhi kutoka kwa wenyeji na kuanzisha miradi ya mifugo au kilimo. Serikali zinaangalia visiwa kama vituo vya manowari zao. Ugawaji wa maeneo ya Pasifiki katika koloni unaanza. Hispania ilitangulia kwa kutawala Ufilipino. Ni hasa Uingereza, Ufaransa, Uholanzi na Marekani wanaojaribu kutawala maeneo, na Ujerumani inaingia mwisho wa karne ya 19. Vita va Marekani dhidi ya Hispania mwishoni mwa karne ya 19 inabadilisha ramani iliyokuwepo awali. Chile inavamia Kisiwa cha Pasaka.

Katika visiwa kadhaa kama Hawaii na Samoa watawala wenyeji walijaribu kupanua madola yao na kushirikiana na wenyeji wengine lakini uwezo wa kijeshi wa Marekani na nchi za Ulaya unashinda.

Ujerumani ilipaswa kuachana na makoloni yake baada ya Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia kufuatana na maazimio ya amani ya Versailles. Japani iliingia kuchukua sehemu ya makoloni yake ya awali.

Katika Vita Kuu ya Pili Japani ilishambulia maeneo yaliyokuwa chini ya Uingereza, Uholanzi, Ufaransa na Marekani na visiwa viliona mapigano makali hadi kushindwa kwa Japani mwaka 1945.

Uhuru tangu miaka ya 1960

[hariri | hariri chanzo]

Baada ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia makoloni ya awali yalipewa nafasi ya kuwa nchi huru au kubaki kama mikoa au majimbo ya nchi za wakoloni wa awali.

Nchi zote zina wakazi wachache; Australia, Nyuzilandi na Papua Guinea Mpya ni mataifa pekee yenye wakazi milioni; pia jimbo la Hawaii la Marekani linapita kiwango hiki. Nchi zote nyingine kwenye visiwa huwa na wakazi lakhi kadhaa au makumi elfu pekee. Hivyo hado leo athira ya majirani makubwa mara nyingi ni muhimu.

Maeneo ambayo hayakuwa nchi huru:

  • Indonesia ilivamia koloni la Guinea Mpya ya Kiholanzi mwaka 1962 wakalazimisha Waholanzi kukabidhi nchi kwao, wakati Uholanzi ilikuwa inawaandaa wazalendo kwa uhuru na maungano na Wapapua wenzao wa mashariki mwa kisiwa. Mwaka 1969 Indonesia iliendesha kura ya wawakilishi wa Wapapua waliowahi kuteua wenyewe iliyokubali kubaki Indonesia.
  • Ufaransa ilifanya koloni lake la Polinesia kuwa eneo la ng'ambo ambako wakazi wote walipewa haki za uraia. Tangu mwaka 2003 kuna "Jumuiya za Kujitawala za Ng'ambo" (collectivité d'outre-mer) mbili ambazo ni Polynesia ya Kifaransa na Wallis na Futuna katika Pasifiki ya kusini. Kaledonia Mpya ina hali ya pekee kama jumuiya ya kujitawala. Wakazi waliitwa mara mbili kulipigia kura swali la kuwa nchi huru. Kura ya mwaka 2020 ilileta asilimia 53 kwa kubaki sehmu ya Ufaransa dhidi asilimia 47 kwa uhuru.
  • Uingereza uliipa Australia na New Zealand haki ya kujitawala tangu karne ya 19; katika karne ya 20 nchi hizo zilipewa haki ya kujitegemea katika sheria zao. Tangu sheria za 1942 na 1947 zimefikia hadhi ya nchi huru zinazoendelea kama wanachama wa Commonwealth kwa hiari yao na kumwa na malkia kama kama mkuu wa nchi.
  • Marekani ilifanya koloni ya Hawaii kuwa jimbo lake sawa na majimbo mengine mnamo 1959. Samoa, Guam na Visiwa vya Mariana ya Kaskazini zinaendelea kama maeneo ya ng'ambo ya Marekani bila haki za kisiasa. Lakini wenyeji wote wana haki kama raia ya Marekani.

Milipuko ya kinyuklia kwenye visiwa

[hariri | hariri chanzo]

Baada ya Vita Kuu ya Pili nchi tatu za Marekani, Ufaransa na Uingereza walitumia maeneo chini ya utawala wao kwa majaribio ya kinyuklia. Bomu la nyuklia liligunduliwa mwisho wa Vita Kuu ya Pili na kutumiwa mara ya kwanza 1945. Katika miaka iliyofuata, nchi kadhaa zililenga kuboresha silaha hizi. Maeneo ya Pasifiki yaliteuliwa kwa milipuko ya majaribio kwa sababu ya idadi ndogo ya wakazi na hali ya kisasa ya maeneo hayo yaliyokuwa makoloni ambako wenyeji hawakuwa na haki za kiraia. Matokeo yalikuwa mara nyingi mabaya kwa wakazi.

  • Marekani ilitumia Visiwa vya Marshall kama uwanja wa majaribio kuanzia 1946 hadi 1958 kwa milipuko ya mabomu 67 ya nyuklia. Bomu la kwanza la haidrojeni ulimwenguni lilijaribiwa katika kisiwa cha Enewetak katika Visiwa vya Marshall mnamo 1 Novemba (tarehe ya hapa) mnamo 1952. Mwaka 1954 wakazi wa atoli ya Rongelap walilazimishwa kuondoka katika kisiwa chao baada ya machafuko wa kinyuklia yalifika kwao kutoka Visiwa vya Marshall. Baada ya miaka mitatu waliurhusiwa kurudi lakini ugonjwa wa saratani ulianza kutokea kati yao kutokana na mnururisho uliobaki kwenye ardhi na maji baada ya milipuko ya kinyuklia.
  • Uingereza iliendesha idadi ya majaribio ya milipuko Australia Kusini katika miaka ya 1950. Waaustralia asilia walilazimishwa kuondoka kwenye nchi za mababu zao.
  • Ufaransa iliwahi kufanya majaribio yake katika jangwa la Algeria. Baada ya uhuru wa Algeria milipuko ilipelekwa Pasifiki ambako Moruroa katika Polynesia ya Kifaransa. Milipuko iliendelea hata baada ya mataifa mengine kusimamisha majaribio juu ya ardhi kwa sababu ya athari mbaya kwa afya. Ufaransa iliendelea dhidi ya ukosoaji na upinzani wa kimataifa; mlipuko wa mwisho hewani ilitokea mnamo 1974, na jaribio la mwisho la chini ya ardhi mnamo 1996.

Kujisomea

[hariri | hariri chanzo]
  • Collingridge, Vanessa (2003). Captain Cook: The Life, Death and Legacy of History's Greatest Explorer. Ebury Press. ISBN 0-09-188898-0.
  • Hough, Richard (1994). Captain James Cook. Hodder and Stoughton. ISBN 0-340-82556-1.
  • Kirch, Patrick Vinton (2001). On the Road of the Winds: An Archaeological History of the Pacific Islands Before European Contact. University of California Press. ISBN 978-0-520-92896-1.
  • Lal, Brij V.; Fortune, Kate (2000). The Pacific Islands: An Encyclopedia. University of Hawaii Press. ISBN 978-0-8248-2265-1.
  • Morison, Samuel Eliot (2001), History of United States Naval Operations in World War II: The rising sun in the Pacific, 1931 – April 1942, University of Illinois Press, ISBN 0-252-06973-0
  • Obeyesekere, Gananath (1992). The Apotheosis of Captain Cook: European Mythmaking in the Pacific. Princeton University Press. ISBN 0-691-05752-4.
  • Obeyesekere, Gananath (1997). The Apotheosis of Captain Cook: European Mythmaking in the Pacific. Princeton University Press. ISBN 978-0-691-05752-1. With new preface and afterword replying to criticism from Sahlins.
  • Sahlins, Marshall David (1985). Islands of history. University of Chicago Press. ISBN 978-0-226-73358-6.
  • Williams, Glyndwr (1997). Captain Cook's Voyages: 1768–1779. London: The Folio Society.
Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Historia ya maeneo ya Pasifiki kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.