Jimbo Katoliki la Same

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta

Jimbo Katoliki la Same (kwa Kilatini Dioecesis Samensis) ni mojawapo kati ya majimbo 33 ya Kanisa Katoliki nchini Tanzania, na kama hayo yote linafuata mapokeo ya Kiroma.

Kanisa kuu liko mjini Same, katika mkoa wa Kilamanjaro na limewekwa wakfu kwa heshima ya Kristo mfalme.

Linahusiana na Jimbo Kuu la Arusha.

Takwimu[hariri | hariri chanzo]

Eneo lake lote ni kama kilometa mraba 10,000, ambamo wamo wakazi 562,950. Kati yao Wakatoliki ni 70,490 (2004) yaani asilimia 12.5.

Waamini hawa wanahudumiwa na mapadri 40, ambao kati yao 35 ni wanajimbo na 5 watawa. Hivyo kwa wastani kila mmojawao anahudumia waamini 1.762.

Parokia ziko 62.

Jimbo lina mabruda 13 na masista 40.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Uongozi[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]