Jimbo Kuu la Arusha

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta

Jimbo Kuu la Arusha (kwa Kilatini Archidioecesis Arushaënsis) ni mojawapo kati ya majimbo 34 (2012) ya Kanisa Katoliki nchini Tanzania na kama hayo yote linafuata mapokeo ya Kiroma.

Chini yake kuna kanda ya Kanisa yenye majimbo yafuatayo: Moshi, Same na Mbulu.

Askofu mkuu wake ni Josaphat Louis Lebulu.

Kanisa kuu liko mjini Arusha na limewekwa wakfu kwa heshima ya Mt. Teresa.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Uongozi[hariri | hariri chanzo]

Takwimu[hariri | hariri chanzo]

Eneo la jimbo lina kilometa mraba 67,340, yaani mkoa wa Arusha na sehemu ya mkoa wa Manyara.

Kati ya wakazi 1,705,687 (2004) Wakatoliki ni 193,446 (sawa na 11.3%) katika parokia 30.

Mapadri ni 86 (42 wanajimbo na 44 watawa), hivyo kwa wastani kila mmojawao anahudumia waumini 2,249.

Pia kuna mabruda 149 na masista 129.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]