VIWAWA
VIWAWA (kifupisho cha Vijana Wakatoliki Wafanyakazi; kwa Kiingereza: Young Christian Workers (YCW; kwa Kifaransa: Jeunesse ouvrière chrétienne) ni chama cha kitume cha Kanisa Katoliki. Makao makuu yako Brussels.
Vijana wa chama hicho wanapatikana kwenye parokia nyingi ulimwenguni na wana umri wa kuanzia miaka 18 hadi 35.
Chama kilianzishwa na padri Joseph Cardijn huko Ubelgiji kikapewa jina hilo mwaka 1924. Kifupisho cha jina la Kifaransa JOC kikawa chanzo cha maneno ya Kiingereza Jocism na Jocist[1].
Mwaka 1925 chama kilipata idhini ya Papa Pius XI, na kuanzia mwaka 1926 kimeenea katika nchi walau 51, ikiwemo Tanzania.
Mwaka 1957 kilikuwa na mkutano wa kwanza wa kimataifa huko Roma.
Cardijn aliendelea kukishughulikia maisha yake yote, akafanywa askofu na kardinali mwaka 1965.
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Jocism", Time, September 26, 1938. Retrieved on 2009-01-22. Archived from the original on 2010-08-26.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- http://www.jociycw.net/ YCW Worldwide
Makala hii kuhusu Kanisa Katoliki bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu VIWAWA kama historia yake au maelezo zaidi? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |