Nenda kwa yaliyomo

Only God Can Judge Me (wimbo)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
"Only God Can Judge Me"
"Only God Can Judge Me" kava
Wimbo wa Tupac Shakur

kutoka katika albamu ya All Eyez on Me

Umetolewa 1995-1996
Umerekodiwa 1996
Aina ya wimbo Hip hop
Urefu 4:57
Studio Death Row Records
Mtunzi Tupac Shakur
Mtayarishaji Doug Rasheed
All Eyez on Me orodha ya nyimbo
  1. "Ambitionz Az a Ridah"
  2. "All Bout U"
  3. "Skandalouz"
  4. "Got My Mind Made Up"
  5. "How Do U Want It"
  6. "2 of Amerikaz Most Wanted"
  7. "No More Pain"
  8. "Heartz of Men"
  9. "Life Goes On"
  10. "Only God Can Judge Me"
  11. "Tradin War Stories"
  12. California Love (Remix)
  13. "I Ain't Mad at Cha"
  14. "What'z Ya Phone #"

"Only God Can Judge Me" ni wimbo kwenye CD ya kwanza (Book One) ya albamu ya All Eyez on Me ya hayati Tupac Shakur. Wimbo unamshirikisha Rappin' 4-Tay na ulirekodiwa wakati Shakur ameingia mkataba na Death Row Records[1]. Huhesabiwa na washabiki kama wimbo wa hali ya juu wa 2Pac.

Wimbo na mashairi

[hariri | hariri chanzo]

Sehemu kubwa ya wimbo inahusu mahusiano ya Shakur na vyombo vya habari. Katika mstari mmoja anasema: "Re-collect your thoughts, don't get caught up in the mix, cause the media is full of dirty tricks", yaani, "tafakari tena na usije ukaingizwa katika mkumbo kwa sababu vyombo vya habari vina njama za kishenzi kibwena".

Kwa ujumla, wimbo una-mgusia maisha yake mwenyewe, na maisha ya dhiki kwa waliokuwa maskini kama yeye ("Thug" alieleza haina maana ya uhuni, bali mtu aliyeishi maisha ya dhiki na baadaye kuja kuwa na hela[2]).

Alisema kwa polisi, "There's a million motherfuckers stressing just like me" na "And they say it's the white man I should fear, but its my own kind doing all the killing here", yaani, "Kuna wajingawajinga kibwena wenye wenye mfadhaiko kama mimi" na "Na wanasema eti Mzungu tu ndiyo ninayepaswa kumwogopa, lakini hapa kipango wangu katika suala zima la kumaliza".

Na baada ya kuelezea kidogo jinsi maisha ya mitaani yanavyoenda, na maisha yake binafsi alivyozoea ndani ya mazingira hayo, viitikio vinakuwa, "Only God can judge me now". Kinachojulikana hasa kwenye wimbo huu ni kwamba Shakur ametabiri hatma yake mwenyewe kwenye wimbo huu, "I hear the doctor standing over me screamin' I can make it, got a body full of bullet holes layin' here naked."

  1. "Tupac-Online.com - Snoop On Tupac And His Effect On His Life". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2010-08-27. Iliwekwa mnamo 2010-05-26.
  2. Tupac: Resurrection