Mkoa wa Morogoro

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru


Mkoa wa Morogoro
Mahali paMkoa wa Morogoro
Mahali paMkoa wa Morogoro
Mahali pa Mkoa wa Morogoro katika Tanzania
Majiranukta: 8°0′S 37°0′E / 8.000°S 37.000°E / -8.000; 37.000
Nchi Tanzania
Wilaya 6
Mji mkuu Morogoro
Serikali
 - Mkuu wa Mkoa Issa Machibya
Eneo
 - Jumla 73,039 km²
Idadi ya wakazi (2002)
 - Wakazi kwa ujumla 1,759,809
Tovuti:  http://www.morogoro.go.tz/

Morogoro ni jina la mji, wilaya na mkoa wa Tanzania.

Mkoa wa Morogoro ni kati ya mikoa 26 ya Tanzania. Umepakana na mikoa ya Tanga, Pwani, Lindi, Ruvuma, Iringa, Dodoma na Arusha. Ikiwa eneo lake ni 72 939 km² kuna wakazi 1,759,809 (mwaka 2002). Morogoro iko kati ya mikoa mikubwa zaidi ya Tanzania.

Utawala

Mkoa una wilaya sita ndizo (idadi ya wakazi kwa mabano): Kilosa ( 489,513), Kilombero (322,779), Morogoro Vijijini (263,920), Morogoro Mjini (228,863), Mvomero (260,525), Ulanga (194,209). Wakazi walio wengi hukalia wilaya za kaskazini mkoani. Robo yao huishi katika miji ya mkoa.

Ramani Wilaya au manisipaa Wakazi (2002) Tarafa Kata Kijiji Eneo km²
Wilaya za Mkoa wa Morogoro
Wilaya za Mkoa wa Morogoro
Wilaya ya Kilombero 321,611 5 19 81 14,918
Wilaya ya Kilosa 489,513 9 37 164 14,245
Wilaya ya Morogoro Vijijini 263,920 6 25 132 11,925
Wilaya ya Morogoro Mjini 227,921 1 19 - 531
Wilaya ya Mvomero 260,525 4 17 101 7,325
Wilaya ya Ulanga 193,280 5 24 65 24,560
Jumla 1,759,809 30 141 543 73,039
Makisio ya idadi ya watu kwa mwaka 2008 ni watu 2,021,714
kutokana na kiwango cha ongezeko la watu la asilimia 2.6 kwa mwaka.
Marejeo: Mkoa wa Morogoro

Eneo

Eneo la Mkoa wa Morogoro liko katikati ya mikoa ya pwani la Bahari Hindi na Nyanda za Juu. Kuna tambarare za chini kama vile Ifakara / Kilombero pia milima ya juu kama Uluguru penye mlima wa Kimhandu mwenye 2646 m juu ya UB.

Mito mikubwa ni Wami na Ruvu inayoanza kwenye milima ya Uluguru. Ruvu ndiyo mto wa kutoa maji ya Daressalaam.

Karibu nusu ya eneo la Mkoa wa Morogoro ni hifadhi za wanyama za Mikumi, Udzungwa na Selous.

Wakazi

Kabila kubwa ni Waluguru waliotoa jina kwa mji wa Morogoro pamoja na milima ya Uluguru. Makabila mengine makubwa zaidi ni Wangulu, Wakagulu, Wasagala na Wapogolo.

Mawasiliano

Barabara Kuu za lami za Daressalaam - Morogoro - Mbeya - Zambia/Malawi na Daressalaam - Morogoro - Dodoma hupita eneo la mkoa pamoja na reli ya kati Daresalaam - Morogoro - Dodoma - Kigoma / Mwanza. Reli ya TAZARA hupita wilaya ya Kilombero.

Uchumi

Kilimo kinategemea hali ya mvua. Kilombero kuna mashamba makubwa ya miwa. Mazao ya sokoni hulimwa milimani. Katibu nusu ya eneo la mashamba yote hulimwa mahindi.


Marejeo ya Nje