Morogoro Vijijini

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Mahali pa Morogoro Vijijini katika mkoa wa Morogoro.

Wilaya ya Morogoro Vijijini ni wilaya moja ya Mkoa wa Morogoro nchini Tanzania. Katika sensa ya mwaka 2002, idadi ya wakazi wa wilaya hiyo ilihesabiwa kuwa 263,920 [1].

Ni wilaya yenye utajiri mkubwa wa hali ya hewa inayoruhusu mazao yote kustawi: mfano, yale ya joto hustawi maeneo ya bondeni, na ya baridi sehemu za milimani. Ni chanzo cha mito inayonywesha Dar-es-Salaam na Pwani. Lakini asilimia kubwa ya wakulima hulima bila faida: hubeba mizigo kwenda sokoni kwa umbali mrefu zaidi ya kilometa 25.

Ni wilaya ya giza,ukiachia Ngerengere jeshini, kulikobaki hakuna lami wala umeme. Wapo watu ambao hawajaona gari tangu kuzaliwa.

Shule zina upungufu mkubwa wa walimu.

Jamii ya wilaya hii ni Waluguru, Wabati, uWakutu, Wandengereko na makabira mengine kutoka mikoa mingine ya Tanzania, Waha, Wasukuma na Wanyatru


Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Flag of Tanzania.svg Kata za Wilaya ya Morogoro vijijini - Tanzania Flag of Tanzania.svg

Bungu | Bwakila Chini | Bwakila Juu | Gwata | Kasanga | Kibogwa | Kibungo Juu | Kidugalo | Kinole | Kiroka | Kisaki | Kisemu | Kolero | Konde (Morogoro) | Lundi | Matuli | Mikese | Mkambalani | Mkulazi | Mkuyuni | Mngazi | Mtombozi | Mvuha | Ngerengere | Selembala | Singisa | Tawa | Tegetero | Tununguo