Mngazi
Mngazi ni kata ya Wilaya ya Morogoro Vijijini katika Mkoa wa Morogoro, Tanzania, yenye Postikodi namba 67226.
Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi walihesabiwa 13,708 [1]. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 9,528 [2] walioishi humo.
Mngazi ni mojawapo kati ya kata zinazounda tarafa ya Bwakira.
Jina la kata linatokana na jina la mto unaopita kijiji kimojawapo kati ya vijiji vinne vinavyounda kata ya Mngazi ambavyo ni: kijiji cha Mngazi, kijiji cha Vigolegole, kijiji cha Milengwelengwe na kijiji cha Sesenga. Jina la mto huo ni Mngazi, nalo limetoa jina la kijiji cha Mngazi.
Mipaka ya kata ya Mngazi ni: kata ya Bwakira Chini kwa upande wa mashariki, kata ya Kisaki kwa upande wa magharibi, kata ya Singisa kwa upande wa kaskazini na hifadhi ya Selous (Selous Game Reserve) kwa upande wa kusini.
Wakazi wengi wa kata ya Mngazi ni Waluguru, Wapogoro, Wakutu, Wambunga na Wandamba.
Upande wa dini, wakazi wa kata ya Mngazi wamegawanyika katika makundi makubwa mawili: Wakristo na Waislamu. Wakristo wengi ni Wakatoliki na wachache Wapentekoste wa kanisa la TAG ambao wengi wao ni wahamiaji.
Shughuli za kiuchumi zinazofanywa katika kata ya Mngazi ni kilimo, ufugaji na biashara ndogondogo zinazotokana na mazao ya kilimo.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ https://www.nbs.go.tz
- ↑ "Sensa ya 2012, Morogoro - Morogoro DC" (PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2016-03-03. Iliwekwa mnamo 2015-03-23.
Kata za Wilaya ya Morogoro Vijijini - Mkoa wa Morogoro - Tanzania | ||
---|---|---|
Bungu | Bwakira Chini | Bwakira Juu | Gwata | Kasanga | Kibogwa | Kibuko | Kibungo | Kidugalo | Kinole | Kiroka | Kisaki | Kisemu | Kolero | Konde | Lundi | Matuli | Mikese | Mkambalani | Mkulazi | Mkuyuni | Mngazi | Mtombozi | Mvuha | Ngerengere | Selembala | Singisa | Tawa | Tegetero | Tomondo | Tununguo |
Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Morogoro bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Mngazi kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. Tafadhali usiingize majina ya maafisa na viongozi wa sasa maana wanabadilika haraka mno. |