Liturujia ya Vipindi
Liturujia ya Vipindi ni sala rasmi ya Kanisa kama inavyoadhimishwa katika madhehebu mbalimbali ya Ukristo, lakini ni jina hasa la mpangilio unaofuatwa na Kanisa la Roma baada ya Mtaguso wa pili wa Vatikano (kwa Kilatini jina ni Liturgia Horarum).
Kwa njia yake wakleri, watawa na waamini wote wa Yesu wa madhehebu hayo wanaungana naye katika sala yake ya kudumu, na wanasaidiwa kuishi kitakatifu saa zote za siku kwa kumkumbuka Mungu mara kwa mara.
Inaitwa hivyo kwa sababu inafanyika kwa vipindi mbalimbali kadiri ya mwendo wa siku (usiku na mchana): muhimu zaidi ni vipindi vya asubuhi (Masifu ya asubuhi) na jioni (Masifu ya jioni), lakini kuna pia vipindi vya usiku kati au alfajiri (Kipindi cha masomo), mchana (Sala ya kabla ya adhuhuri, Sala ya adhuhuri na Sala ya baada ya adhuhuri) na kabla ya kulala (Sala ya mwisho).
Katika Kanisa la Kilatini hiyo sala ya Kanisa inategemea hasa Biblia ya Kikristo kwa kutumia Zaburi na masomo kutoka kwake.
Matini yake yote yamekusanywa pamoja katika kitabu kimoja ambacho kwa sababu hiyo kilizoeleka kuitwa breviari (yaani: "matini kwa ufupi", badala ya kuzagaa katika vitabu mbalimbali kama zamani).
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]Makala
[hariri | hariri chanzo]- "General Instruction" from the Breviary Ilihifadhiwa 5 Januari 2015 kwenye Wayback Machine.
- The Divine Office: A Study of the Roman Breviary Ilihifadhiwa 21 Novemba 2008 kwenye Wayback Machine. by the Rev. E.J. Quigley
- EWTN article on the Liturgy of the Hours / Divine Office / Breviary Ilihifadhiwa 9 Julai 2019 kwenye Wayback Machine.
- 1911 Catholic Encyclopedia
- Discovering Prayer: How to Pray the Liturgy of the Hours by Seth H. Murray (also available with audio samples)
- Breviary Timeline – A timeline of official 20th century breviaries
- How to Pray the Daily Office from the Book of Common Prayer Ilihifadhiwa 2 Machi 2010 kwenye Wayback Machine.
Matini na sauti
[hariri | hariri chanzo]- Societas Laudis: Liturgia Horarum – Chanted Liturgy of the Hours, daily broadcast by Radio Vaticana
- DivineOffice.org – Full Text and Audio Liturgy of the Hours website, podcast and apps supporting a large prayer community.
- Universalis – an online version of the current Catholic Liturgy of the Hours, in English
- Divinum Officium – an online dynamic version of the Breviarium Romanum according to the rubrics of 1960
- Liturgia Horarum Online An online version of the Liturgy of the Hours.
- The Roman Breviary (1954 edition) Ilihifadhiwa 17 Oktoba 2010 kwenye Wayback Machine. (Latin with English translation in an adjoining column)
- Daily Office of the Roman Catholic Church According to the Anglican Use – Online version of the Daily Office from the Book of Divine Worship an ecclesiastically approved variant on the Roman Rite of the Catholic Church.
- The Anglican Breviary – Anglican version of the Daily Office
- Liturgia Horarum Online Online Liturgy of the Hours in Latin
- Liturgia Horarum in cantu Gregoriano Ilihifadhiwa 26 Juni 2010 kwenye Wayback Machine. – Online Gregorian chants for the Liturgy of the Hours in Latin
- The Daily Office sung at the Community of Jesus (non-denominational) Ilihifadhiwa 26 Juni 2014 kwenye Wayback Machine.
Miongozo
[hariri | hariri chanzo]- CLAA Weekly Guide to the Liturgy of the Hours Ilihifadhiwa 12 Oktoba 2014 kwenye Wayback Machine. – A detailed daily guide to praying the Liturgy of the Hours. Free subscription.
- General Instructions of the Liturgy of the Hours – Rubrics for Liturgy of the Hours
Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Liturujia ya Vipindi kama historia yake, matokeo au athari zake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |