Nenda kwa yaliyomo

Bad (wimbo)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
“Bad”
“Bad” cover
Single ya Michael Jackson
kutoka katika albamu ya Bad
Imetolewa 7 Septemba 1987
Muundo CD single
Imerekodiwa 1987
Aina Funk, Dance-Pop
Urefu 4:06
Studio Epic Records
Mtunzi Michael Jackson
Mtayarishaji Michael Jackson na Quincy Jones
Mwenendo wa single za Michael Jackson
"I Just Can't Stop Loving You"
(1987)
"Bad"
(1987)
"The Way You Make Me Feel"
(1987)

Bad kilikuwa kibao kilichotamba kunako mnamo 1987 ambacho kilirekodiwa na msanii wa muziki wa pop Michael Jackson. Kibao hiki kilikuwa cha pili katika vitano kuingia kwenye chati za Billboard Hot 100 na kushika nafasi ya kwanza kwa albamu ya Bad, na kilikuwa kibao chake cha saba kushika nafasi ya saba.[1]

Kuhusiana na wimbo

[hariri | hariri chanzo]

Kiasili, wimbo huu uliandaliwa ili uimbwe kwa pamoja na Prince, msanii mwenye uzoefu wa miaka mingi, ambaye alitarajiwa kuchangia mistari yake. Katika mahojiano, Quincy Jones alieleza kuhusu tukio hili katika toleo maalumu la Bad, akisema kwamba Prince alimwambia Jackson hakuwa na nia ya kushiriki kwa sababu “wimbo utakuwa maarufu hata bila mimi kushiriki.” Mnamo mwaka wa 1996, katika mahojiano na televisheni ya Kijerumani, Prince alifafanua kwamba sababu ya kutoshiriki ilikuwa mstari wa kwanza uliosema “Your butt is mine”. Kwa hilo, Jackson alijibu: “Siwezi kusema hivyo kwako… na wewe pia huwezi kuniambia hivyo!”

Katika kitabu chake cha mwaka wa 1988 kiitwacho Moonwalk, Jackson aliandika kwamba Bad ni wimbo unaohusiana na maisha ya mtaani. Anaeleza kuwa unahusu vijana wanaotoka katika familia zenye changamoto, ambao hupata nafasi ya kusoma katika shule za heshima lakini hatimaye hurudi mitaani. Anaporudi, anakumbana na vikwazo kutoka kwa vijana wa mtaani. Ndipo anauliza kwa uimbaji: “Mimi mbaya, wewe mbaya, nani mbaya, je, ni nani mwema?” Jackson anaeleza kwamba unapokuwa thabiti na jasiri, basi ujue wewe ndiye “mbaya.”

Mnamo mwaka wa 2006, single hii, na video yake, zilitolewa tena zikiwa kama moja ya sehemu ya toleo la Visionary - The Video Singles.

Pefomansi ya kati

[hariri | hariri chanzo]
Chati (1987) Nafasi
iliyoshika
U.S. Billboard Hot 100 1
Australian Kent Music Report 4
Belgian Singles Chart 1
Canadian Singles Chart 1
Danish Singles Chart 1
Uholanzi Singles Chart 1[2]
French Singles Chart 4
German Singles Chart 2
Irish Singles Chart 1
Italian Singles Chart 5
Norwei's Singles Chart 2
Swedish Singles Chart 4
Swiss Singles Chart 3[3]
UK Singles Chart 3
Chati (2009) Nafasi
iliyoshika
Australian Singles Chart 27
Austrian Singles Chart 38
Danish Singles Chart 37
Irish Singles Chart 33
Swiss Singles Chart 15[3]
UK Singles Chart 40
U.S. Billboard Hot Digital Songs[4] 23

Orodha ya nyimbo

[hariri | hariri chanzo]

Toleo halisi

[hariri | hariri chanzo]
UK 7" single
  1. "Bad" (7" single mix) – 4:06
  2. "Bad" (Dance Remix Radio Edit) – 4:54
UK 12" single
  1. "Bad" (Dance Extended Mix Includes 'False Fade') – 8:24
  2. "Bad" (Dub version) – 4:05
  3. "Bad" (A cappella) – 3:49
U.S. CD single
  1. "Bad" (Dance Extended Mix Includes "false fade") – 8:24
  2. "Bad" (7" single mix) – 4:06
  3. "Bad" (Dance Remix Radio Edit) – 4:54
  4. "Bad" (Dub version) - 4.05
  5. "Bad" (A cappella) – 3:49

Toleo la Visionary

[hariri | hariri chanzo]
CD single
  1. "Bad" (7" single mix) - 4:06
  2. "Bad" ("False Fade" Dance Extended Mix) - 8:22
DVD single
  1. "Bad" (Music video)
  1. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-07-03. Iliwekwa mnamo 2009-07-20.
  2. "De Nederlandse Top 40, week 40, 1987". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-01-18. Iliwekwa mnamo 2008-03-16.
  3. 1 2 "Swiss Singles Chart Archives". hitparade.ch. Iliwekwa mnamo 18 Julai 2009.
  4. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-07-04. Iliwekwa mnamo 2009-07-20.
Makala hii kuhusu mambo ya muziki bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Bad (wimbo) kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.