Bad

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Bad
Bad Cover
Studio album ya Michael Jackson
Imetolewa 31 Agosti 1987
Imerekodiwa Novemba 1986Julai 1987 (kasoro Another Part of Me: ilirekodiwa 1985)
Aina Soul, R&B, Dansi-pop, Urban, Pop rock[1]
Urefu 48:16
Lebo Epic
EK-40600
Mtayarishaji Michael Jackson,
Quincy Jones[2]
Tahakiki za kitaalamu
Wendo wa albamu za Michael Jackson
Thriller
(1982)
Bad
(1987)
Dangerous
(1991)
Single za kutoka katika albamu ya Bad
  1. "I Just Can't Stop Loving You"
    Imetolewa: 20 Julai 1987
  2. "Bad"
    Imetolewa: 7 Septemba 1987
  3. "The Way You Make Me Feel"
    Imetolewa: 9 Novemba 1987
  4. "Man in the Mirror"
    Imetolewa: 9 Januari 1988
  5. "Dirty Diana"
    Imetolewa: 18 Aprili 1988
  6. "Another Part of Me"
    Imetolewa: 11 Julai 1988
  7. "Smooth Criminal"
    Imetolewa: 24 Oktoba 1988
  8. "Leave Me Alone"
    Imetolewa: 13 Februari 1989
  9. "Liberian Girl"
    Imetolewa: 3 Julai 1989

Bad ni jina la kutaja albamu ya saba ya mwanamuziki, mtayarishaji wa rekodi, mwimbaji, mfanyabiashara, kabaila, na mhisani wa Kimarekani, Michael Jackson. Albamu ilitolewa mnamo tar. 31 Agosti 1987 na studio ya Epic/CBS Records. Rekodi ya albamu hii ilitolewa karibuni miaka mitano tangu kutoka kwa albamu ya awali. Miaka ishirini baada ya kutolewa, albamu imeuza takriban nakala zaidi ya milioni 30 kwa dunia nzima, na kopi milioni 8 ziliuzwa nchi za nje kwa kupitia Marekani peke yake. Bad ni albamu ya kwanza, na ndiyo hadi sasa albamu pekee, iliyoweza kuingiza single tano katika Billboard Hot 100 zikiwa nafasi ya 1.[3]

Katika albamu hii, Jackson ameonekana kuwa huru zaidi kupita zile albamu zake za mbili za awali, Off the Wall na albamu yenye mauzo bora kwa muda wote, Thriller. Humu katunga nyimbo tisa katika kumi na moja za albamu, na amesaidia kutunga na kutayarisha wimbo wa "Man in the Mirror". Pia humu amekuja na sura mpya ya mshangao.

Albamu iliendelea kupata mafanikio makubwa katika miaka ya 1980 na imeshinda tuzo mbili za Grammy, moja kwa Muziki Bora wa Video - Leave Me Alone na nyingine kwa ajili ya Uhandisi Bora wa Albamu, Bruce Swedien na Humberto Gatica.[4] Mnamo mwaka 2009, Bad pia, imewekwa nafasi ya 43 katika orodha ya Albamu Bora 100 za Karne za MTV zilizoorodheshwa na VH1.[5] Albamu pia iliwekwa nafasi ya 202 katika orodha ya gazeti ya Rolling Stone, Albamu Bora ya Karne.[6]

Historia[hariri | hariri chanzo]

Orodha ya nyimbo[hariri | hariri chanzo]

# JinaMtunzi (wa) Urefu
1. "Bad"  Michael Jackson 4:07
2. "The Way You Make Me Feel"  Jackson 4:58
3. "Speed Demon"  Jackson 4:03
4. "Liberian Girl"  Jackson 3:53
5. "Just Good Friends" (kaimba na Stevie Wonder)Terry Britten, Graham Lyle 4:08
6. "Another Part of Me"  Jackson 3:54
7. "Man in the Mirror"  Glen Ballard, Siedah Garrett 5:19
8. "I Just Can't Stop Loving You" (kaimba na Siedah Garrett)Jackson 4:13
9. "Dirty Diana"  Jackson 4:40
10. "Smooth Criminal"  Jackson 4:17
Toleo la CD la 1988
# JinaMtunzi (wa) Urefu
11. "Leave Me Alone"  Jackson 4:38
"Toleo Maalumu" la 2001 [7]
# JinaMtunzi (wa) Urefu
12. "Interview with Quincy Jones #1"    4:03
13. "Streetwalker" (Awali haikutolewa)Jackson 5:49
14. "Interview with Quincy Jones #2"    2:53
15. "Todo Mi Amor Eres Tu" (Toleo la Kihispania la "I Just Can't Stop Loving You", awali haikupatikana)Jackson, Rubén Blades 4:05
16. "Interview with Quincy Jones #3"    2:30
17. "Spoken intro to Fly Away"    0:08
18. "Fly Away" (Awali haikutolewa)Jackson 3:26

Toleo la pili la Bad limekuwa na utofauti fulani ukifananisha na lile toleo la mwaka wa 1987:[8]

  • "Bad" inabadiliko ya utayarishaji.
  • "The Way You Make Me Feel" ina utajiri wa sauti za nyuma kuliko ya awali.
  • "I Just Can't Stop Loving You" imeondosha maneno ya mwanzo ya Jackson.
  • "Dirty Diana" imeongezeka kidogo.
  • "Smooth Criminal" imeondosha pumzi za kigiizaji na intro.

Single zake[hariri | hariri chanzo]

  1. Julai 1987 - "I Just Can't Stop Loving You" U.S. #1 / UK #1
  2. Septemba 1987 - "Bad" U.S. #1 / UK #3
  3. Novemba 1987 - "The Way You Make Me Feel" U.S. #1 / UK #3
  4. Januari 1988 - "Man in the Mirror" U.S. #1 / UK #21
  5. Aprili 1988 - "Dirty Diana" U.S. #1 / UK #4
  6. Julai 1988 - "Another Part of Me" U.S. #11 / UK #15
  7. Septemba 1988 - "Smooth Criminal" U.S. #7 / UK #8
  8. Januari 1989 - "Leave Me Alone" UK #2
  9. Juni 1989 - "Liberian Girl" UK #13[9]

Chati zake[hariri | hariri chanzo]

Chati (1987) Nafasi
iliyoshika
Australia 2
Austria 1
Brazil 1
Kanada 1
Ufaransa 1
Ujerumani 1
Italia 1
Japani 1
Uholanzi 1
New Zealand 1
Norwei 1
Sweden 1
Switzerland 1
UK Albums Chart 1
U.S. Billboard 200 1
U.S. R&B/Hip-Hop Albums 1

Matunukio[hariri | hariri chanzo]

Nchi Matunikio Nchi za nje
Australia 5x Platinamu 350,000
Austria 4x Platinamu 80,000 [10]
Brazil Diamond 1,100,000
Kanada 7x Platinamu 700,000
Ufaransa Almasi 1,400,000
Ujerumani 4x Platinamu 2,000,000
Japani Almasi 1,000,000
Hispania 7x Platinamu 500,000
UK 13x Platinamu 3,600,000
U.S. 8x Platinamu 8,100,000

Mauzo ya Marekani[hariri | hariri chanzo]

Kipindi Tuzo ya RIAA Kupeleka nchi za nje kutoka U.S. Jumla
Aug 31, 1987 - Nov 9, 1987 Gold, Platinum na 3x Platinum mnamo Nov 9, 1987 3,000,000 3,000,000
Nov 10, 1987 - Dec 31, 1987 4x Platinum mnamo Dec 31, 1987 1,000,000 4,000,000
Jan 1, 1988 - Mar 21, 1988 5x Platinum mnamo Mar 21, 1988 1,000,000 5,000,000
Mar 22, 1988 - Jun 1, 1988 6x Platinum mnamo Jun 1, 1988 1,000,000 6,000,000
Jun 2, 1988 - Aug 25, 1993 7x Platinum mnamo Aug 25, 1993 1,000,000 7,000,000
Aug 26, 1993 - Sep 29, 1994 8x Platinum mnamo Sep 29, 1994 1,000,000 8,000,000

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Bad. AllMusic. Iliwekwa mnamo 2009-04-27.
  2. Album Credits for Bad. Artists Direct. Jalada kutoka ya awali juu ya 2009-07-14. Iliwekwa mnamo 3 Februari 2006.
  3. MTV - Michael Jackson Biography
  4. Grammy for Bruce Swedien & Humberto Gatica. Grammy. Jalada kutoka ya awali juu ya 2009-06-20. Iliwekwa mnamo 2009-02-25.
  5. Bowman, Edith. VH1 - Greatest Albums Ever. VH1. Jalada kutoka ya awali juu ya 2009-03-10. Iliwekwa mnamo 9 Aprili 2009.
  6. The RS 500 Greatest Albums of All Time. Rolling Stone. Jalada kutoka ya awali juu ya 2008-06-23. Iliwekwa mnamo 18 Novemba 2003.
  7. Bad/Dangerous. www.amazon.co.uk. Iliwekwa mnamo 2008-08-25.
  8. Michael Jackson: Kwa upande wa rekodi. Chris Cadman, Michael Haystead.
  9. Michael Jackson , The Ultimate Collection, Booklet
  10. IFPI Austria - Verband der Österreichischen Musikwirtschaft

Maelezo[hariri | hariri chanzo]

Tazama[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]