Ghosts (video)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ghosts
Imeongozwa na Stan Winston
Imetayarishwa na Michael Jackson
Stan Winston
David Nicksay
Imetungwa na Michael Jackson
Stephen King
Nyota Michael Jackson
Mos Def
Muziki na Michael Jackson
Imesambazwa na Kingdom Pictures
Imetolewa tar. 9 Mei 1997
Ina muda wa dk. 39:31
Lugha Kiingereza
Bajeti ya filamu Haijulikani

Ghosts ni filamu fupi iliyofanywa na Michael Jackson na iliongozwa na mwongozaji wa filamu na mtaalamu wa vionjo maalumu vya filamu, Stan Winston. Filamu hii au video hii imetjwa kuwa ni miongoni mwa video ndefu sana. Ilipigwa na na kutupwa kwenye matv mnamo mwaka 1996 na ilitolewa ikiwa pamoja na filamu ya Stephen King's THINNER. Ilikuja kutolewa tena kimataifa baada ya mwaka mmoja baadaye na kwenye VHS.

Filamu inaelezea hadithi ya bwana mmoja mwenye nguvu za giza, ambaye alilazimishwa kuuhama mji na meya wa mjini hapo. Filamu inajumlisha mfululizo mzima wa utaratibu wa kucheza muziki uliofanywa na Michael Jackson na "familia" yake ya mashetani. Kila wimbo kwenye filamu hii umechukuliwa kutoka kwenye albamu yake ya HIStory na Blood on the Dance Floor. Filamu hii pia ni mashahuri kwa kuwa ndiyo mara ya kwanza kuonekana kwa msanii wa maigizo/rapa na filamu wa Kimarekani Mos Def.

Hadithi[hariri | hariri chanzo]

Bwana mchawi (Jackson) anaishi peke yake kwenye jumba linaloonekana tupu lililopo juu ya kilele cha mlima, linaangalia mji wa "Normal Valley" kwa chini. Wakati huohuo, anawaburudisha watoto wa mjini kwa mazingaombwe madogomadogo ya kutisha. Mmoja kati ya watoto wale akamweleza mama yake, ambaye ndiye aliyeenda kumjulisha bwana Meya (pia imechezwa na Jackson); akajichukua yeye na watu wa mjini pale na kwenda kwa yule Bwana mchawi na kumtaka aondoke mjini pale. Mmoja kati ya wale alionekana kutotaka kufanya hivyo, lakini alitiwa msukumo na Meya ili ajiunge kundini.

Usiku wa giza uliojawa na radi wakaingia kwenye jumba la yule Bwana mchawi (ambamo badala ya kwenda sehemu walionyeshwa badala yake wamekwenda "Sehemu Nyingine") wakiwa wameshika kandili za moto. Pindi walipofika kwenye jumba hilo, jumba ilinalindwa bonge la geti la chuma. Wakapenya getini, na wakiwa na macho ya wasiwasi katika jumba hilo, wakapata wazo la pili la kuingia ndani kabisa. Watoto wakawa wanawahakikishia wazazi wao kwamba Bwana mchawi hakufanya jambo baya kabisa, na kuwaomba wazazi kwamba kama vipi waachane naye tu. Lakini Meya akasikia na kusema, "Yule ni kituko, na hakuna sehemu mjini hapa kwa ajili ya vituko!".

Wakiwa wanakaribia geti la mbele la jumba lile likafunguka, jambo ambalo liliwatisha wanakijiji wale, ambao walikuwa wakipata mwongozo wap kwa kupitia mlango wa mbele, ambao pia ulijifungua wenyewe. Ndani ya jumba kunaonekana kunatisha sana kwao kuliko hata kule nje walipotoka, na wazazi wakaanza kuwahusia watoto wao (na wao wenyewe) kwamba "hakuna kitu kama hicho cha kusema vizuka". Wakawa wanaendelea kuongoza kule ndani zaidi, na pindi walipofika wote ndani kabisa, mlango wa barazani ukajibamiza na kujiloki wenyewe.

Milango mikubwa miwili ilifunguka na kubainika kuwa ni mikubwa sana, ndani kiza kinene kwenye ukumbi. Kwa kusita, wanakijiji wale wakawa wanaeleka wenyewe kwenye eneo la ukumbi wa kuchezea, ambapo walisalimiwa na Bwana mchawi ambaye alikuwa bado anawatisha na vimadawa vya moshi pale pa kuingilia. Meya akawa na jazba naye na kumfanyia fujo, na kuthubutu kumwita yule Mchawi "kumbe cha ajabu", "kituko", na "anatisha", na kumweleza kwamba hakaribishwi kabisa katika mji wao. Yule mchawi akaanza kujitetea, na kujibu vitisho vya Meya kwamba "Utaondoka mwenyewe, ama unataka nikujeruhi?" (Watu wa mjini pale wakaonekana wanataka kujiharishia, lakini hawakuruhusiwa kutoa pingamizi).

Kwa jambo hili yule Bwana mchawi akajibu, "Unajaribu kunitisha, siyo?...Naona sasasina jinsi; Inanibidi nikutishe na wewe." Baada ya hapo akaanza kufanya vituko na mizaha vya uso kwa mfululizo, kitendo ambacho Meya aliita "upuuzi" na "siyo mzaha". Kwa kubadilisha sauti, Bwana mchawi akauliza, "Hili nalo linatisha?" Na kulivuta sura lake juu na chini kabla hajalinyoosha domo lake sawa. Kisha akawa anaendelea kulinyulula sura lake zaidi, kwa haraka zaidi kalivuta lile sura hadi kujifichua lile sura lake na kuwa mifupa mitupu na kuanza kucheka kimzaha. Vitisho hivyo vilipelekea wanakijiji wale kukimbilia mlangoni, ambamo Bwana mchawi akaifunga milango yote kwa kutumia nguvu zake za kichawi, kisha akavusha sura yake ya mifupa kwa kutumia mikono yake, na kuanza kuonyesha sura yake ya kawaida.

Baada ya muda Bwana mchawi akawatambulisha wanakijiji kwa "familia" yake ya majini, wakiwa pamoja na Bwana mchawi, wakaanza kucheza muziki kwa utaratibu (muziki kamili uliotuingwa na Jackson) ambao uliwatisha wanakijiji na muda huohuo kuwaburudisha. Wakati wa kipengele hicho kinaendelea, Bwana mchawi akaanza kuvua nguo na kuonyesha mwili wake wa ndani ambao ni mifupa mitupu; akamwingia Neya mwilini na kumchezesha; na kumbadilisha Meya kuja kwenye sura baya, sura la shetani la kutisha huku likisema, "Nani kinyambolelo sasa?" ," Unachekesha, Unachekesha".

Baada ya onyesho kwisha, Bwana mchawi akauliza, "Bado mnanitala niondoke?". Wanakijiji wakajibu "hapana", Meya akajibu kwa mihasira "Ndiyo!". Bwana mchawi akakubali kuondoka kwa unyonge na kusema, "Sawa...Nitaondoka." Akaaunguka chini, na akaanza kujivunja mikono yake kwenye sakafu sura lake na mwili lake likaanza kupagalanyika na kuchukua na upepo. Wanakijiji wale waliuzunishwa na hili, na kuanza kujisikia huruma kwa kuondoka kwake. Baada ya hili Meya akafikiria kwamba amekuja na ushindi na kuanza kuongoza njia ya kuelekea mlangoni na huku akisema "Nimemwonyesha kudadadeki zake". Alipofungua mlango tu kakutana na bonge la sura la Bwana mchawi pale mlnagoni huku likisema "HELLO" na kumshitua kweli, na akaanza kukimbia kwa woga (na kuanza alama za vioo vya sehemu ambayo Meya alipita kwa kasi kwenye milango ya vioo).

Wanakijiji wale wakaenda kufungua mlango na kumwona Bwana mchawi kasimama kule, wakajichekesha. Wakagundua kwamba si mtu mbaya na kuanza kutaka amani naye. Hadithi inaishia madogo wawili wamebebana huku wakiwa wamevaa vazi na sura la kutisha na kumwuliza Bwana mchawi, "Hii inatisha?"; akashtuka na kuwa na sura ya upole kabisa, na kujibu "Hapana!" Baada ya hapo kamera ikahamishwa na kusika makelele makali kwa mbali yakisika ndani ya jumba hilo.

Washiriki[hariri | hariri chanzo]

 • Bwana uchawi/Meya/Meya Jini/Jini refu/Mifupa mitupu - Michael Jackson
 • Watu wa mjini pale ni:
  • Kendall Cunningham
  • Pat Dade
  • Mos Def
  • Dale Dudeck
  • Heather Ehlers
  • Shawnette Heard
  • Edwina Moore
  • Shana Mangatal
  • Loren Randolph
  • Amy Smallman
  • Seth Smith
  • Leonard A. Anderson

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]