Singapuri
Singapuri |
---|
Singapuri ni nchi ndogo katika Asia ya Kusini-Mashariki.
Jiografia[hariri | hariri chanzo]
Eneo lake ni kisiwa kwenye ncha ya kusini kabisa ya Rasi ya Malay pamoja na visiwa vidogo vya kando. Kisiwa kimetenganishwa na bara kwa mfereji mwembamba wa Johor.
Kuna mji mmoja tu: ni jiji la Singapuri lilipopo kisiwani, hivyo huhesabiwa pia kati ya dola-miji.
Historia[hariri | hariri chanzo]
Kisiwa kiliwahi kuwa na makazi mbalimbali katika historia. Mji wa kisasa ulianzishwa mwaka 1819 na Waingereza kama kituo cha biashara ikawa bandari muhimu ya eneo.
Uingereza uliipa uhuru kama sehemu ya shirikisho la Malaysia. Lakini matatizo ya kuelewana yalionekana haraka kati ya wanasiasa Wamalay wa bara na wenzao Wachina wa kisiwani.
Mwishowe Singapuri ikafukuzwa katika shirikisho ikawa nchi ya kujitegemea tarehe 9 Agosti 1965. Mwanasiasa Lee Kuan Yew alikuwa waziri mkuu wa kwanza akaendelea na cheo hiki hadi mwaka 1990 akaongoza Singapuri kuwa kati ya mataifa matajiri ya Asia.
Wakazi[hariri | hariri chanzo]
Kati ya wakazi milioni tano na nusu walio wengi (74.3%) ni wa asili ya China. Mababu wao walihamia huko wakitafuta kazi bandarini.
Wengine ni wakazi asilia Wamalay (13.5%) na Watamil na wengineo waliotokea Uhindi (9%).
Kuna lugha 24 ambazo huzungumzwa nchini Singapuri. Lugha rasmi ni Kiingereza (48.3%), Kichina (38.6%), Kimalay (9.2%) na Kitamil (2,5%).
Upande wa dini, 31.1% ni Wabuddha, 18.9% ni Wakristo, 15.6% ni Waislamu, 8.8% ni Watao, 5% ni Wahindu.
Uchumi[hariri | hariri chanzo]
Uchumi wa Singapuri unategemea zaidi biashara, hasa benki pamoja na viwanda.
Imekuwa kitovu cha uchumi na biashara kwa Asia ya Kusini.
Tazama pia[hariri | hariri chanzo]
Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]
- (Kiingereza) Tovuti rasmi
- Serikali
- Singapore Government Directory Interactive
- Singapore Government Online Portal
- Gateway To All Government Services Archived 16 Septemba 2018 at the Wayback Machine.
- Singapore National Service Portal
- Singapore Accounting and Corporate Regulatory Authority
- Chief of State and Cabinet Members[dead link]
- Singapore Economic Development Board
- Taarifa za jumla
- Singapore entry at The World Factbook
- Singapore Archived 7 Juni 2008 at the Wayback Machine. from UCB Libraries GovPubs
- Singapuri katika Open Directory Project
- Singapore profile from the BBC News
- Singapore at Encyclopædia Britannica
- Singapore: Background and U.S. Relations Archived 20 Aprili 2014 at the Wayback Machine. Congressional Research Service
- Singapore Infomap
- Wikimedia Atlas of Singapore
- WikiSatellite view of Singapore at WikiMapia
- Official Gateway To Singapore Archived 5 Juni 2010 at the Wayback Machine.
- Official Singapore Tourism Website
- Key Development Forecasts for Singapore from International Futures
- Biashara
Nchi na maeneo ya Asia |
Afghanistan | Armenia2 | Azerbaijan | Bahrain | Bangladesh | Bhutan | Brunei | China | Falme za Kiarabu | Georgia2 | Hong Kong3 | Indonesia | Iraq | Israel | Jamhuri ya China (Taiwan) | Japani | Kamboja | Kazakhstan | Kirgizia | Korea Kaskazini | Korea Kusini | Kupro2 | Kuwait | Laos | Lebanoni | Macau3 | Malaysia | Maldivi | Mongolia | Myanmar | Nepal | Omani | Pakistan | Palestina | Qatar | Saudia | Singapuri | Sri Lanka | Syria | Tajikistan | Timor ya Mashariki | Turkmenistan | Uajemi | Ufilipino | Uhindi | Urusi1 | Uthai | Uturuki1 | Uzbekistan | Vietnam | Yemen | Yordani |
1. Nchi ina maeneo katika Asia na Ulaya. 2. Nchi iko Asia lakini inahesabiwa pia kati ya nchi za Ulaya kwa sababu za historia au utamaduni. 3. Eneo la pekee la China. |
Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Singapuri kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |