Turkana (ziwa)
3°35′N 36°7′E / 3.583°N 36.117°E
| |
Mahali | Afrika ya Mashariki |
Nchi zinazopakana | Kenya (Ethiopia ina pembe ya kaskazini kabisa) |
Eneo la maji | km² 6.405 |
Kina cha chini | m 73 |
Mito inayoingia | Omo, Turkwel, Kerio na mingine mingi |
Mito inayotoka | -- |
Kimo cha uso wa maji juu ya UB |
375 m |
Miji mikubwa ufukoni | (vijiji vichache tu) |
Ziwa Turkana ni ziwa kubwa lililopo katika kaskazini yabisi ya Kenya. Halina mto unaotoka, hivyo maji yanayoingia yanapotea kwa njia ya uvukizaji. Kwa jumla ni ziwa la Kenya lakini ncha ya kaskazini iko ndani ya Ethiopia. Ni pia ziwa la jangwani liliko kubwa kuliko yote duniani.
Eneo na tabia za ziwa
[hariri | hariri chanzo]Umbo la ziwa ni kama kanda ndefu inayoelea kutoka kaskazini kwenda kusini. Urefu wa ziwa ni kilomita 290, upana wake hadi kilomita 32. Eneo la maji ni km² 6,405. Ndani ya ziwa kuna visiwa vitatu vidogo vinyavoitwa Kisiwa cha kusini, cha kati na cha kaskazini.
Turkana ni ziwa la magadi lakini maji yake hunywewa na watu na wanyama na yanawezesha viumbehai wengi kuishi ndani yake.
Hifadhi za wanyama kwenye ziwa Turkana zimeorodheshwa na UNESCO kama Urithi wa Dunia, zikiwemo Hifadhi ya Taifa ya Sibiloi (mashariki kwa ziwa), Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Kati na Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Kusini (visiwani).
Mazingira hayo yote yanahatarishwa sasa na ujenzi wa lambo la Gilgel Gibe III kwenye mto Omo unaochangia ziwa kwa kiasi kikubwa.
Jina
[hariri | hariri chanzo]Wenyeji wametumia majina mbalimbali kufuatana na lugha zao. Waturkana hutumia "anam Ka'alakol" yaani "ziwa la samaki wengi". Wapelelezi Wazungu wa karne ya 19 walisikia jina la "Basso Narok" ingawa haieleweki hii ilikuwa lugha gani.
Kimataifa ziwa lilijulikana zamani kwa jina la "Ziwa Rudolph" (Rudolfsee, Lake Rudolph) lililotolewa na mpelelezi Mhungaria Sámuel Teleki kwa heshima ya mtemi Rudolph, mtoto wa mfalme wa Austria-Hungaria.
Visiwa vinavyopatikana katika ziwa hilo
[hariri | hariri chanzo]- Kisiwa cha Kaskazini (kaunti ya Turkana)
- Kisiwa cha Kati
- Kisiwa cha Ekinyang (kaunti ya Marsabit)
- Kisiwa cha Enwoiti (kaunti ya Marsabit)
- Kisiwa cha Kusini (kaunti ya Marsabit)
- Kisiwa cha Nan (kaunti ya Marsabit)
- Kisiwa cha Nanet (kaunti ya Marsabit)
Mito inayochangia ziwa
[hariri | hariri chanzo]Kutoka Ethiopia
[hariri | hariri chanzo]Mto wa kwanza kabisa katika kuchangia ziwa Turkana (90% hivi) uko upande wa Ethiopia: ni mto Omo (na matawimto yake na ya mito midogo zaidi inayoyachangia, kama Mto Usno, Mto Mago, Mto Neri, Mto Mui, Mto Mantsa, Mto Zigina, Mto Denchya, Mto Gojeb, Mto Gibe, Mto Gilgel Gibe, mto Amara, mto Alanga, Mto Maze na Mto Wabe. Miaka mingine Mto Kibish pia unafikia ziwa hilo.
Kutoka Kenya
[hariri | hariri chanzo]Mito mingine mingi inachangia pia ziwa Turkana upande wa Kenya, ingawa si kwa kiasi kile cha mto Omto; ni hii ifuatayo: • Mto Abelibel • Mto Aberit • Mto Aguli • Mto Ainabkoi (ziwa Turkana) • Mto Aino • Mto Aiye Nai-Anginyang-Kiporr • Mto Akaderte • Mto Akatelyan • Mto Akatwan • Mto Akeriemet • Mto Akhurya • Mto Akiriamet • Mto Akope • Mto Akores • Mto Akouaekori • Mto Akukuth • Mto Alale • Mto Alamonges • Mto Alelalokeya • Mto Alongolomoi • Mto Amelaromuryankol • Mto Amunyai • Mto Anam • Mto Anamuton • Mto Ananoi • Mto Angamojak • Mto Angaro • Mto Angmatia • Mto Angorangora • Mto Anomat • Mto Anyagalim • Mto Apaigiron • Mto Apow • Mto Arau • Mto Arionomur • Mto Aroga • Mto Arorr • Mto Arorr (West Pokot) • Mto Asasum • Mto Atead • Mto Aterr • Mto Atir • Mto Atot • Mto Auanaparan • Mto Ayonai Aterr • Mto Ayonaialopakalumong • Mto Barawa • Mto Barua • Mto Buleth • Mto Cheberen • Mto Cheberkeriungo • Mto Cheborgo • Mto Chekolatom • Mto Chemeri • Mto Chemeroi • Mto Chemonges • Mto Chemosusu • Mto Chemwapit • Mto Chepareria • Mto Chepkobeh • Mto Chepkondol • Mto Chepkuloi • Mto Chepolol • Mto Chepropoi • Mto Cheptak • Mto Cheptandan • Mto Cheptilon • Mto Cherial • Mto Chesabet • Mto Chesera • Mto Chesoi • Mto Chiapan • Mto Chukulukong • Mto Didinga • Mto Dupas • Mto Ekebekebyeke • Mto Ekwapalopyot • Mto Emaniman • Mto Emanit • Mto Embamachukwa • Mto Embamon • Mto Embasos • Mto Embobit • Mto Embogh • Mto Embomoruk • Mto Embong' • Mto Empungung • Mto Emsea • Mto Emso • Mto Enbenye • Mto Endo • Mto Endogh • Mto Enopogh • Mto Enumpapa • Mto Epuryamudang • Mto Eron • Mto Erron • Mto Etebusait • Mto Etionin • Mto Gachiengur • Mto Ganathawaole • Mto Gateruk • Mto Gochobolok • Mto Goisoi • Mto Gurgur • Mto Habokok • Mto Iang • Mto Ikalotonyang • Mto Ineletum • Mto Iryionomoch • Mto Jaban • Mto Kaabilikeret • Mto Kaabole • Mto Kaakwor • Mto Kaaling • Mto Kaangole • Mto Kaapus • Mto Kaaronikagiete • Mto Kaawat • Mto Kabanyet • Mto Kabarait • Mto Kabelangole • Mto Kabokuli • Mto Kabwangederr • Mto Kabyen • Mto Kachakarimoch • Mto Kachalakin • Mto Kachar • Mto Kachoda • Mto Kachoke • Mto Kachuro Mongin • Mto Kadingetom • Mto Kadoupokimak • Mto Kaekalkiryon • Mto Kaekudokol • Mto Kaemasekin • Mto Kaeri Akak • Mto Kaetako • Mto Kagiro • Mto Kai-Ekongo • Mto Kaiboni • Mto Kaichom • Mto Kaiechech • Mto Kaiegilai • Mto Kaiekoropus • Mto Kaiekunyang • Mto Kaiekunyuk • Mto Kaiemute • Mto Kaikirr • Mto Kaikoba • Mto Kaikor • Mto Kaimo • Mto Kainyangakok • Mto Kainyangalok • Mto Kaiothin • Mto Kaitakalchwel • Mto Kaitio • Mto Kajukujuk • Mto Kakalel • Mto Kakedmosing • Mto Kakelai • Mto Kakiporomwoi • Mto Kakore • Mto Kakumio • Mto Kakurio • Mto Kakuroetom • Mto Kakwe • Mto Kalabata • Mto Kalabata (korongo la Turkana) • Mto Kalachir • Mto Kalain • Mto Kalakol • Mto Kalatum • Mto Kalempus • Mto Kalewa • Mto Kalimarok • Mto Kalimhaun • Mto Kalochoro • Mto Kalokerith • Mto Kalokhole • Mto Kalokodo • Mto Kalokoel • Mto Kalokopirr • Mto Kalonyangkori • Mto Kalopeto • Mto Kaloponogole • Mto Kalorith • Mto Kalorukongole • Mto Kalosia • Mto Kalotiman • Mto Kalotumokoi • Mto Kaloyapamugie • Mto Kamarethi • Mto Kamarlei • Mto Kamila (West Pokot) • Mto Kamodo • Mto Kamogoro • Mto Kamuma • Mto Kanaiki • Mto Kanaki • Mto Kanamukuin • Mto Kanangor • Mto Kanaodon • Mto Kanaro • Mto Kanathuwat • Mto Kang'wak • Mto Kangachin • Mto Kangaki • Mto Kangakurio • Mto Kangalemo • Mto Kangebet • Mto Kangetet (Turkana) • Mto Kangibenyoi • Mto Kangimedr • Mto Kangisirite • Mto Kangoli • Mto Kanguwapeta • Mto Kanigiyum • Mto Kanugurumeri • Mto Kanyangareng • Mto Kao (Turkana) • Mto Kapchebu • Mto Kapchepgero • Mto Kapelikori • Mto Kaperarengam • Mto Kapeta • Mto Kapim • Mto Kapkobe • Mto Kapleel • Mto Kapsang • Mto Kaptarit • Mto Kapua • Mto Karamuroi • Mto Kare-Kapakalem • Mto Kareburr • Mto Karkal • Mto Karubangorok • Mto Karunkyukuri • Mto Kasaguru • Mto Kataboi • Mto Kateruk • Mto Kathunguru • Mto Katik • Mto Katikithikiria • Mto Katiko • Mto Katirikiki • Mto Katirr • Mto Katmerit • Mto Katupe • Mto Kaupa • Mto Kauriong' • Mto Kauriung • Mto Kawala (Turkana) • Mto Kawalathe • Mto Kawalathi • Mto Kawianguli • Mto Kayekongai • Mto Keesigiria • Mto Kemaguriat • Mto Kerio (korongo) • Mto Kerio • Mto Keris • Mto Keritunet • Mto Keryemeryeme • Mto Kesok • Mto Kianantuing • Mto Kibaas • Mto Kibaino • Mto Kibereget • Mto Kibiemit • Mto Kiblabot • Mto Kiken • Mto Kimaguhir • Mto Kinoinoi • Mto Kipkanyilat • Mto Kipsang • Mto Kipsiwara • Mto Kiptalyung • Mto Kiptunol • Mto Kirumbopso • Mto Kobothan • Mto Kochar • Mto Kochodin • Mto Kochokio • Mto Kochuch • Mto Koduaran • Mto Kogene • Mto Kokiselei • Mto Kokithelei • Mto Kokolopit • Mto Kokoten • Mto Kokothelei • Mto Kokothowa • Mto Kokure • Mto Kolok • Mto Kolomokori • Mto Kolonyadarsh • Mto Komakatae • Mto Komen Angalio • Mto Komocheri • Mto Kopatia • Mto Kopedo • Mto Kopeto • Mto Kopuai • Mto Kordei • Mto Korinyang • Mto Kortokoil • Mto Kosibirr • Mto Kotaruk • Mto Kothiai • Mto Kotome • Mto Kunyao • Mto Kurumboni • Mto Lachoa Achila • Mto Laga Sapari • Mto Laga Tulu-Bor • Mto Laisamis • Mto Laminkwais • Mto Lawawet • Mto Lazuli • Mto Lelean • Mto Lenchukuti • Mto Let • Mto Loarengak • Mto Lobokat • Mto Loborio • Mto Loburet • Mto Lochan • Mto Locharakhiang • Mto Locheremoit • Mto Lochil • Mto Lochore-Angdapala • Mto Lochoro • Mto Lochurututu • Mto Lochwai • Mto Loge • Mto Logogo • Mto Logum • Mto Loitan • Mto Loiya • Mto Lokalale • Mto Lokapetemoi • Mto Lokedule • Mto Loketi • Mto Lokhosinyakhori • Mto Lokichar • Mto Lokidongo • Mto Lokimyel • Mto Lokiporrangithikiria • Mto Lokirikipi • Mto Lokitoinyala • Mto Lokomoru • Mto Lokoparaparai • Mto Lokopel • Mto Lokore • Mto Lokorikipi • Mto Lokosima-ekori • Mto Lokucho • Mto Lokuso • Mto Lokwakipi • Mto Lokwamur • Mto Lokwanamoru • Mto Lokwathinyon • Mto Lokwatubwa • Mto Lolii • Mto Lolim • Mto Lolmorton • Mto Lomeiyen • Mto Lomekwi • Mto Lomelo • Mto Lomunyan-Akirichok • Mto Lomunyenakwan • Mto Lomuryamuge • Mto Long'enya • Mto Longeleiya • Mto Longinya • Mto Loochuk • Mto Loolimo • Mto Loolung • Mto Loparokowayen • Mto Loperichich • Mto Lopiripira • Mto Lopotwa • Mto Lopuroto • Mto Loreng • Mto Lorengaloup • Mto Lorugumu • Mto Lotepakiru • Mto Lothajait • Mto Lotiman • Mto Lotirai • Mto Lotongot • Mto Lotukales • Mto Lowotha • Mto Lowoyegweli • Mto Loya • Mto Loyai Engole • Mto Lukwakore • Mto Luturut • Mto Macheremowe • Mto Makurinya • Mto Malmalte • Mto Mamchor • Mto Mamponich • Mto Marchaui • Mto Maricha • Mto Marie Mokale • Mto Marin • Mto Marso • Mto Marun • Mto Masei • Mto Mboo Sangarao • Mto Mindi • Mto Mkorwa • Mto Mogorua • Mto Moinoi • Mto Monti • Mto Morok • Mto Mortorth • Mto Mugurr • Mto Munyen • Mto Munyen (korongo) • Mto Murua Nyaap • Mto Murukirion • Mto Musgut • Mto Naalimatumak • Mto Nabar • Mto Nabelete Akoit • Mto Nabergoit • Mto Nabukut • Mto Nabwalekorot • Mto Nachalal • Mto Nachedet • Mto Nachoo • Mto Nachukui • Mto Nachurokaali • Mto Nadopua • Mto Naedakal • Mto Naekitoenyala • Mto Naeyepunetebu • Mto Nagaramoroi • Mto Nagitokonok • Mto Nagola • Mto Nagomolkipik • Mto Nagum Napala • Mto Naichetarukoin • Mto Naijokore • Mto Nairepon • Mto Naitangro • Mto Naithilum • Mto Naiyena • Mto Naiyena Angilimo • Mto Naiyena Aregae • Mto Naiyena Ekalale • Mto Naiyena Enyathanait • Mto Naiyena Kabaran • Mto Naiyenaelim • Mto Naiyenai Atulela • Mto Naiyenai Kororon • Mto Nakabothan • Mto Nakadongot • Mto Nakalalai • Mto Nakalale (korongo) • Mto Nakapeliowoi • Mto Nakaterretai • Mto Nakaton • Mto Nakatoni • Mto Nakauron • Mto Nakayot • Mto Nakejuamothing • Mto Nakeridan • Mto Nakerikan • Mto Nakeroman • Mto Nakilima • Mto Nakilowonok • Mto Nakipomye • Mto Nakito-Konon • Mto Nakitonguro • Mto Nakoret • Mto Nakuijit • Mto Nakurio • Mto Nakuwotom • Mto Nakwakal • Mto Nakwamosing • Mto Nakwee • Mto Nakwehe • Mto Nakwei • Mto Nalepet • Mto Nalibamun • Mto Namaniko • Mto Namejanit • Mto Nameturan • Mto Namuroi • Mto Nanamakali • Mto Nangamanat • Mto Nanukor • Mto Naoiatuba • Mto Naoiyapie • Mto Naon • Mto Napas • Mto Napaton • Mto Napeichom • Mto Napeitanit • Mto Napeitau • Mto Napiot • Mto Naporoto • Mto Napow • Mto Narengmor • Mto Nariokotome • Mto Narodi • Mto Narototin • Mto Narubu • Mto Nasorr • Mto Natapara • Mto Nathagait • Mto Nathekuna • Mto Nathura • Mto Nathuruken • Mto Natieket • Mto Natir • Mto Natira (Kenya) • Mto Natome • Mto Natoo • Mto Natudau • Mto Natumamong • Mto Nauruto • Mto Nawakiring • Mto Nawaton • Mto Nawoiaekalale • Mto Nayanae Koorin • Mto Nderemon • Mto Ngakile • Mto Ngatagoin • Mto Ngilimo • Mto Ngipurryo • Mto Ngiputire • Mto Ngirengo • Mto Ngombei • Mto Ngrombwe • Mto Nguapet • Mto Nguruthio • Mto Ninyit • Mto Nitelejor • Mto Niteleyo • Mto Nyaparei • Mto Nyikim • Mto Okilim • Mto Oleyapare • Mto Orengaloup • Mto Oropoi • Mto Pechipet • Mto Perekon • Mto Pesik • Mto Pongung • Mto Pulichon • Mto Reberwa • Mto Riritian • Mto Rogoch • Mto Sagat • Mto Samakitok • Mto Samuke • Mto Sasame • Mto Sebit • Mto Sergoi (West Pokot) • Mto Sergothwa • Mto Seruach • Mto Siga (West Pokot) • Mto Sikawa • Mto Sinjo • Mto Siwa • Mto Sostin • Mto Sowayan • Mto Suam • Mto Suguta (Kenya) • Mto Tamabero • Mto Tamass • Mto Tamogh • Mto Tangasia • Mto Terik • Mto Thapet • Mto Thoro • Mto Tindarr • Mto Tirken • Mto Tiya • Mto Toperrnawi • Mto Torok • Mto Tugha • Mto Turkwel • Mto Tusa (ziwa Turkana) • Mto Tutuwei • Mto Uluguthe • Mto Wei Wei • Mto Yemenin • Mto Yeptos
Kutoka Uganda
[hariri | hariri chanzo]Mito ifuatayo kutoka Uganda inachangia pia ziwa Turkana kupitia Kenya: Mto Arionomunyen, Mto Chosan, Mto Ekiringura, Mto Kacholese, Mto Kalodurr, Mto Kalopomongole, Mto Kanyagareng, Mto Komongim, Mto Koromoich, Mto Laburin, mto Lobuloyin, Mto Lochorakwangen, Mto Lodias, Mto Loitabela, Mto Lomapus, Mto Lopedot, Mto Naakot, Mto Nabunei, Mto Nakakerikeri, Mto Nakalale, Mto Nakatuman, Mto Namusio, Mto Nangolipia, Mto Natire, Mto Naunyet, Mto Nauyagum, Mto Onogin na Mto Otiko.
Kutoka Sudan Kusini
[hariri | hariri chanzo]Mito mingine inayochangia ziwa hilo inaanzia Sudan Kusini, hasa mto Kibish.
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Turkana (ziwa) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |