Kerio (mto)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Bonde la Kerio

Kerio ni mto wa mkoa wa Bonde la Ufa nchini Kenya. Chanzo chake kiko karibu na ikweta kwenye mitelemko ya ngome ya Elgeyo (Keiyo) kwenye kimo cha karibu mita 2,000.

Mto hufuata mwendo wake katika bonde la Kerio ambalo ni sehemu ya Bonde la Ufa kubwa. Mto huelekea kaskazini kati ya milima ya Elgeyo na milima ya Tugen ukipita katika Marakwet na Pokot mashariki hadi kuishia katika Ziwa Turkana.

Kerio ni kati ya mito mirefu ya Kenya.