Turkana (ziwa)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Ziwa Turkana
Ziwa Turkana
Ziwa Turkana
Mahali Afrika ya Mashariki
Nchi zinazopakana Kenya (Ethiopia ina pembe ya kaskazini kabisa)
Eneo la maji 6.405 km²
Kina ya chini 73 m
Mito inayoingia Omo, Turkwel na Kerio
Mito inayotoka --
Kimo cha uwiano wa maji juu ya UB 375 m
Miji mikubwa ufukoni (vijiji vichache tu)

Ziwa Turkana ni ziwa katika kaskazini yabisi ya Kenya. Halina mto unaotoka, hivyo maji yanayoingia yanapotea kwa njia ya uvukizaji. Ni ziwa kubwa la Kenya lakini ncha ya kaskazini iko ndani ya Ethiopia. Ni pia ziwa la jangwani liliko kubwa kuliko yote duniani.

Umbo la ziwa ni kama kanda ndefu linaloelea kutoka kaskazini kwenda kusini. Urefu wa ziwa ni kilomita 290, upana wake hadi kilomita 32. Eneo la maji ni km² 6,405. Ndani ya ziwa kuna visiwa vitatu vidogo vinyavoitwa Kisiwa cha kusini, cha kati na cha kaskazini.

Turkana ni ziwa la magadi lakini maji yake hunywewa na watu na wanyama.

Jina[hariri | hariri chanzo]

Ziwa Turkana linavyoonekana kutoka angani.

Wenyeji wametumia majina mbalimbali kufuatana na lugha zao. Waturkana hutumia "anam Ka'alakol" yaani "ziwa la samaki wengi". Wapelelezi Wazungu wa karne ya 19 walisikia jina la "Basso Narok" ingawa haieleweki hii ilikuwa lugha gani.

Kimataifa jina lilijulikana kwa jina la "Ziwa Rudolph" (Rudolfsee, Lake Rudolph) lililotolewa na mpelelezi Mhungaria Sámuel Teleki kwa heshima ya mtemi Rudolph, mtoto wa mfalme wa Austria-Hungaria.

Africa satellite plane.jpg Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Turkana (ziwa) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.