Mkoa wa Mwanza

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru


Mkoa wa Mwanza
Mahali paMkoa wa Mwanza
Mahali paMkoa wa Mwanza
Mahali pa Mkoa wa Mwanza katika Tanzania
Majiranukta: 2°45′S 32°45′E / 2.750°S 32.750°E / -2.750; 32.750
Nchi Tanzania
Wilaya 8
Mji mkuu Mwanza
Serikali
 - Mkuu wa Mkoa Abas Kandoro
Eneo
 - Jumla 19,592 km²
Idadi ya wakazi (2002)
 - Wakazi kwa ujumla 2,942,148
Tovuti:  http://www.mwanza.go.tz/

Mkoa wa Mwanza ni kati ya mikoa 26 za Tanzania. Umepakana na Kagera upande wa magharibi, Shinyanga upande wa kusini na Mara upande wa mashariki. Ziwa la Viktoria Nyanza liko kaskazini. Makao makuu ya mkoa yapo Mwanza mjini.

Wilaya

Mkoa wa Mwanza una wakazi 2,942,148 (sensa ya 2002) katika wilaya 8 ukiwa na eneo la 19,592 km2. Wilaya ndizo Ukerewe, Magu, Sengerema, Geita, Misungwi, Kwimba, Nyamaganga na Ilemela. Jiji la Mwanza lina ndani yake wilaya za Nyamagana na Ilemela.

Ramani (kabla ya 2012) Wilaya au manisipaa Wakazi (2022) Tarafa Kata Kijiji Eneo km²
Wilaya za Mkoa wa Mwanza
Wilaya za Mkoa wa Mwanza
Wilaya ya Buchosa 413,110
Wilaya ya Ilemela 509,687
Wilaya ya Kwimba 480,025
Wilaya ya Magu 421,119
Wilaya ya Misungwi 467,867
Wilaya ya Nyamagana 594,834
Wilaya ya Sengerema 425,415
Wilaya ya Ukerewe 387,815
Jumla 3,699,872
Marejeo: Mkoa wa Mwanza

Wakazi

Makabila makubwa katika Mwanza ndio Wasukuma, Wakerewe, Wakara na Wazinza.

Viungo vya nje