Bara la Antaktiki

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Antaktiki (kijani) katika ramani ya dunia.
Antaktiki kutoka angani.
Kituo cha kisayansi katika Antaktiki.

Antaktiki ni bara lililopo kwenye ncha ya kusini ya dunia.

Jina "Antaktiki" linatokana na lugha ya Kigiriki likimaanisha "kinyume cha Aktiki", ambapo Aktiki ni eneo karibu na ncha ya kaskazini.

Takriban 98% za eneo la bara limefunikwa na theluji na barafu.

Kwa sababu ya baridi kali katika bara hilo, ni bara pekee ambako binadamu hawaishi kwa namna ya kudumu, isipokuwa kuna watu 5,000, hasa wanasayansi, wanaokaa kwa muda katika vituo vyao.

Mtoto wa kwanza kuzaliwa barani huko alizaliwa mwaka 1984. Kwa sasa kuna shule kadhaa na kanisa moja.

Eneo lake ni kubwa kushinda Ulaya lakini hakuna mti hata mmoja. Bara hili linajulikana kama jangwa baridi.

Bara liko kati ya bahari za Pasifiki, Atlantiki na Bahari Hindi.

Kuna volkeno hai moja inayotema moto baraniː ni mlima wa Mount Erebus.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Sciences de la terre.svg Makala hii kuhusu eneo fulani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Bara la Antaktiki kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.