Roald Amundsen

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Meli "Belgica" ya Amudsen ikifungwa katika barafu wakati wa safari yake ya kwanza kuelekea Antaktiki mwaka 1898


Roald Engebreth Gravning Amundsen (* 16 Julai 1872 Borge (leo: Fredrikstad - Norwei; † mnamo 18 Juni 1928 katika Aktiki) alikuwa mpelelezi Mnorwei aliyekuwa mtu wa kwanza wa kufikia Ncha ya kusini mwaka 1911.

Kabla ya hayo alikuwa mtu wa kwanza aliyefaulu kuvuka mpito wa kaskazini-magharibi kati ya Atlantiki na Pasifiki katika miaka 1903 - 1906.

Katika safari mbalimbali alikuwa pia mtu wa kwanza aliyevuka Aktiki na ncha ya kaskazini hewani kwa kutumia ndegeputo mwaka 1926.

Alikufa 1928 kwenye Aktiki alipojaribu kumwokoa mpelelezi Mwitalia aliyekuwa alipotea katika barafu.